Na Kija Elias, Moshi
HALMASHAURI ya wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro,
imetoa onyo kali kwa walimu wakuu wa skuli za msingi wilayani humo, ambao
wamekuwa na tabia ya kuwatoza fedha wazazi pindi wanapofuatilia cheti cha
kuhitimu darasa la saba watoto wao.
Agizo hilo
limetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Moris Makoi, wakati
alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la halmashauri hiyo,
ambapo alisema wapo baadhi ya wazazi wamekuwa wakitozwa kiasi cha shilingi
10,000, na walimu wakuu wa skuli za msingi ili waweze kuwapatia vyeti hivyo.
Mwenyekiti huyo wa halmashauri, alimtaka Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri hiyo, Fulgence Mponji, kuwaandikia barua za onyo kali kwa
walimu ambao wamekuwa na tabia za kuwatoza wazazi fedha ili waweze kuwapatia
vyeti hivyo.
“Yapo malalamiko ya wazazi kutozwa fedha na walimu
wakuu wa skuli za msingi katika wilaya yetu, na malalamiko haya yamenifikia
ofisini kwangu, na baraza hili linakuagiza kuwaandikia barua za onyo walimu
wanaowatoza fedha wazazi wanaofuatailia cheti cha kumaliza darasa la saba,
kwani kwa kufanya hivyo wanaichafulia sifa halmashauri yetu,”alisema Makoi.
Alisema kitendo cha walimu wakuwatoza kiasi hicho cha
fedha kwa lengo la kuwapatia cheti hakipo katika halmashauri yetu, na kwamba
vyeti hivyo hutolewa bure na serikali hivyo mzazi anapofuatilia cheti cha mtoto
wake ni vyema akapewa bure na si vinginevyo.
Kwa upande wao baadhi ya Madiwani ambao walipata fursa
ya kuchangia maoni walihoji uhalali wa mzazi kutozwa fedha ndipo apatiwe cheti
cha mototo wake, ambapo pia walitaka kujua fedha ambazo wamekuwa wakizitoa
zinapelekwa wapi hata wanapodai risiti hawapewi.
“Kuna mchezo mchafu ambao unafanywa na walimu wakuu
kwenye shule za msingi, mzazi anapokwenda shuleni kwa ajili ya kupata cheti cha
motto wake aliyemaliza darasa la saba anatozwa fedha tena shilingi 10,000,
ambayo haina maelezo yeyote yale,” walisema Madiwani hao.
Akijibu malalamiko hayo, Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo, alisema kuwa hakuna uhalali wa kutozwa na kwamba maelekezo ya
wizara ni kwamba cheti hicho hutolewa bure na hakilipiwi kama
ambavyo wanafanya walimu hao.
No comments:
Post a Comment