Na Laylat Khalfan
POLISI jamii Mkoa wa Mjini Magharibi, imesema kuoengezeka kwa
makosa ya uhalifu Mkoani humo kunachangiwa na Wananchi kuwaficha wahalifu wa makosa hayo.
Kamanda Mkaguzi wa polisi jamii mkoa wa Mjini Magharibi,
Mohammed Ramadhan, alisema hayo katika ziara ya kutembelea vituo vya ulinzi
shirikishi katika shehia za mkoa huo.
Alisema kuwa baadhi ya Wananchi wana tabia ya kufumbia macho
matatizo yanayojitokeza kwenye maeneo yao
yakiwemo utumiaji wa dawa za kulevya na vitendo vya ubakaji.
Aidha alisema kuwa endapo Wananchi watakuwa na ushirikiano wakutosha
na jeshi la polisi basi kwa kiasi kikubwa uhalifu utapungua katika jamii na
kuweza kuleta maendeleo.
Kamanda huyo alisema Wanachi wanapaswa kushirikiana na jeshi
la polisi katika kukomesha vitendo viovu kwa kutoa taarifa za watu wanaowatilia
mashaka.
Aidha alifahamisha makosa mengine yaliyojitokeza ni pamoja uuzaji
wa dawa za kulevya mtaa wa Kundemba ambao unachukuliwa kama
soko kuu la biashara hiyo.
“Ni jambo la kushangaza sana
jinsi ulivyo mtaa wa kundemba yaani kazi yao
kubwa ni kujishirikisha na mambo maovu ambayo yanasababisha kurudisha nyuma
mendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla”alisema Mkuu huyo.
Alieleza polisi jamii amejipanga kuweka mikakati madhubuti
ambayo itasaidia kukomesha vitendo vya uvunjani amani nchini.
Kamanda mkaguzi usisingizie wananchi kutokuwataja wahalifu. Hapa kwetu siku hizi wasio name makosa ndio wanaokamatwa na kubambikiziwa kesi za ajabu ajabu. Wale wenye kustahiki kukamatwa ndio wanaotanua mitaani name kufanya hayo maovu. Kwanini mushindwe kuwakamata wahuni wavuta Bangi name wauza unga pale Kundemba wakati we we mwenyeo umethibitisha kuwepo kwa wahalifu hao? Mumuzoea kuonea wanyonge wa mungu name kuwaacha wahuni mitaani then munasingizia eti wananchi. Mbona mukiwataka hao wanyonge munawakamata majumbani mwao usiku? Yana mwisho haya!
ReplyDelete