Na Khamisuu Abdallah
ASKARI Polisi wa Kikosi cha Valantia Zanzibar (KVZ), amefariki dunia baada ya vespa aliyopanda
kuacha njia na kugonga mti katika maeneo ya Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar .
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo , Ofisini kwake Muembemadema Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mjini Magharibi Mkadam Khamis Mkadam wakati akizungumza na mwandishi wa habari
hizi alisema tukio hilo
lilitokea Agosti 5 mwaka huu majira ya saa 4:30 za usiku.
Aidha kamanda Mkadam alimtaja askari huyo kwa
jina la Juma Ameir Pandu (30) ambae ni askari polisi wa kikosi hicho na kueleza
kuwa aliumia sana
sehemu za kichwani na kufariki dunia mara tu baada ya kufikishwa Hospitali kuu
ya Mmnazimmoja na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.
Alisema ajali nyengine ilitokea Agosti 6
mwaka huu majira ya saa 9:20 jioni huko Kinazini Backlays na kusababisha kifo
cha kijana Rajab Ali Makame (38) mkaazi wa Amani Wilaya ya Mjini Unguja.
Alisema ajali hiyo ilihusisha vespa yenye
namba za usajili Z 293 AD iliyokuwa ikiendeshwa na kijana Juma Omar Mussa (49)
mkaazi wa Darajabovu baada ya kuigonga kwa nyuma gari yenye namba za usajili Z
316 CU P/H iliyokuwa mbele yao
ikiendeshwa na Miraji Makame Hassan (36) mkaazi wa Mpendae waliokuwa wakielekea
upande wa Saateni.
Hata hivyo alisema katika ajali hiyo
vijana hao waliumia na kwa bahati mbaya Rajab ambae alipakiwa alipata madhara
makubwa kichwani kwake na kupotaza damu nyingi hadi kusababisha kifo chake.
Hivyo Kamanda Mkadam aliwataka madereva
wanaondesha vyombo vya moto hasa vya maringi mawili kuvaa kofia maalum ambazo
zitakuwa ili kunusuru vichwa vyao.
No comments:
Post a Comment