Na
Othman Khamis, OMPR
MAKAMU
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, amesema viongozi wa kidini
wanapaswa kuwa macho kuzikataa choko choko na ushawishi unaotolewa na wanasiasa.
Alisema
kazi inayotakiwa kufanywa na viongozi hao ni kuwaombea watu wakiwemo viongozi
wa nchi ili baraka ziongezeke ndani ya taifa pamoja na umma jambo ambalo
litasaidia kupunguza misuguano.
Alisema
hayo wakati akilifungua tamasha la kuliombea taifa na kuhamasisha amani,
linalofanyika ukumbi wa Masai Laugwa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Alisema
amani na utulivu wanaojivunia Watanzania miaka mingi sasa ni miongoni mwa neema
zinazopaswa kutumiwa vizuri.
Alisisitiza
njia nzuri ya kuzitumia neema hizo ni kwa wananchi kuzidisha juhudi katika
uzalishaji mali wiwandani na mashambani, kuzidisha upendo na mshikamano bila ya
kujali rangi, kabila au asili ya mtu.
Aliitahadharisha
jamii kutotoa nafasi kwa watu wenye nia mbaya ya kutaka kuliangamiza taifa na kulitumbukiza
kwenye vurugu na mapigano.
“Mimi
kamak wa serikali kwa kushirikiana na viongozi wenzangu na wananchi wenye nia
njema na taifa letu tutaendelea kufanya kazi wakati wote na tutahakikisha amani
na utulivu inadumu
ndani ya nchi yetu ambayo ndio maisha yetu,” alisema.
Alitoa
wito kwa akina mama kuendelea kuwa walinzi na
wasimamizi wa amani na utulivu.
Alisema
mara nyingi wanawake na watoto ndio waathirika wakubwa wa vurugu, hivyo amani
ndio suluhisho pekee la
kuwalinda.
“Mara
nyingi tunashuhudia kwenye vyombo vya habari jinsi wanawake na watoto
wanavyokufa au kujeruhiwa kutokana na
vita vinavyozuka katika maeneo yao,”
alisema.
Akizungumzia
dawa za kulevya ambazo ni tishio a vijana, alisema serikali inachukua juhudi
kupambana na janga hilo.
Alisema
serikali zote mbili zinachukua hatua za makusudi katika viwanja vya ndege na bandari
kwa kuwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu na kupunguza kasi ya
uingizaji.
Aliwaomba
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi ili kuwabaini
wahusika wakuu wa mtandao wa
biashara hiyo.
Alilipongeza
kanisa la Restoration kwa jitihada linazochukua kuokoa maisha ya vijana
walioathirika na dawa za kulevya.
Mapema
Askofu Sedrick Ndonde wa kanisa hilo, alisema taifa limekuwa na cheche
hatarishi inayoonekana kuchochea choko
choko za kidini, kisiasa pamoja na
vitendo vya kigaidi.
Alisema
hali hiyo inayokwenda sambamba na matumizi ya dawa za kulevya inasababisha mfumko
wa uhalifu unaowafanya wananchi waendelee kuishi katika maisha ya hofu.
No comments:
Post a Comment