Na
Masanja Mabula, Pemba
VIONGOZI
wa kamati ya maadili na Mashekhe katika shehia ya Tumbe, wamesema hakuna mvuvi
aliyefukuzwa ama kuzuiwa kuvua na kuuza samaki katika bandari ya Tumbe.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi, wamekanusha taarifa zinazotolewa na baadhi ya
wavuvi kwamba wamefukuzwa na kuzuiwa kuvua na kuuza samaki katika bandari hiyo na
kusema walichozuia ni kuuza samaki wa kuzamia wakati wa mwezi wa Ramadhani.
Walisema
kutokana na imani za kidini ni kosa kuzamiwa wakati wa Ramadhani na kusisitiza
kwamba wananchi wa Tumbe wako tayari kushirikiana na wavuvi wanaokuja kwa
shughuli za uvuvi katika bandari yao lakini uamuzi wa kuzuia kuuza samaki wa
kuzamia kila ifikapo Ramadhani uko pale
pale.
Katibu
wa Kamati ya maadili, Seif Juma, alisema kabla hawajachukua hatua za kuzuia
kuuzwa samaki wa kuzamia katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani, walikutana na
wavuvi waliokuweko dago na kuwataka wasiuze samaki wanaowavua kwa njia hiyo.
"Sisi
hatukukurupuka, kwanza tulikutana na wavuvi mwezi 28 kabla ya Ramadha ni,
tulifanya hivyo ili kulinda na kuheshimu mwezi wa Ramadhani tunashangaa kusikia
wamefukuzwa,” alisema.
Naye
Shekhe Mbwana Dawa, alisema kwa mujibu wa dini ya kiislamu, Waislamu wametakiwa
kuchukia mabaya yanayotendeka machoni au kuyakataza kwa mikono na kwamba
wanaozamia swaumu zao hazikubaliki.
Katibu
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Tumbe, Sharif Ali Khamis, aliwataka wavuvi kuheshimu
makubaliano yaliyofikiwa na kusema taarifa za kufukuzwa na kuzuiwa kuuza samaki
si za kweli.
Alisema
wananchi wa Tumbe wanatambua mchango wa sekta ya uvuvi katika kuchangia pato la
taifa na wananchi wake na kuwataka wavuvi kuondoa dhana hiyo potofu.
No comments:
Post a Comment