Na Kija Elias, Moshi
Jjeshi la Polisi limewataka
wananchi kutoa taarifa sahihi juu ya uhalifu ambao umekuwa ukijitokeza nchini.
Kauli hiyo imetolewa na IGP,
Ernest Mangu, wakati akizindua kituo cha polisi Majengo, Wilaya ya Moshi Mkoani
Kilimanjaro, kilichokarabatiwa kwa nguvu
za wananchi, ambapo zaidi ya shilingi milioni 44 zimetumika.
“Jeshi la polisi haliwezi kulinda raia na mali
zao kama hakuna ushirikiano baina ya wananchi na jeshi hili,hivyo ninachowaomba
wananchi muendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi,”alisema.
Alisema suala la uhalifu bado
ni tatizo kubwa, hivyo aliwataka wananchi
kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuweza kupunguza uhalifu huo.
Alimwagiza Kamanda wa mkoa wa
Kilimanjaro, Robert Boas, kuhakikisha kituo hicho kinatoa huduma bora bila ya
kuwa na upendeleo kwa wananchi, kwani ndilo deni ambalo wananchi wamelikabidhi
kwa jeshi hilo.
Aliwataka wananchi kutoa
taarifa za askari polisi wanaojihusisha na vitendo viouvu ili aweze kuwachukulia
hatua ikiwa ni pamoja na kuwafukuza.
Katika hatua nyingine, IGP
Mangu, alipata fursa ya kuzindua jengo la dawati la jinsia na watoto la wilaya
ya Moshi ambalo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 117.
Awali kitoa taarifa kwa Mkuu wa
polisi nchini, Kaimu Kamanda wa mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita, alisema kituo hicho
kilijengwa enzi za mkoloni, hivyo kilikuwa kinavuja wakati mvua zinaponyesha na
kushindwa kutoa huduma.
No comments:
Post a Comment