Na
Mahmoud Ahmad
Halmashauri ya jiji la Arusha ipo mbioni kukifanya kituo cha afya cha Lovolosi kuwa hospitali
ya jiji kwa kupanua majengo yake na kuweka vifaa tiba vya kisasa lengo likiwa
kuwapatia huduma bora za afya wakazi wa jiji hilo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Juma Iddy, alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea mikakati ya kusogeza huduma za
kijamii karibu na wananchi.
Alisema
hatua hiyo inakuja baada ya jiji kufungua kituo cha afya cha daraja mbili
chenye uwezo wa kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 19,000 wa kata za Daraja
Mbili,Sokon 1,Lemara na maeneo ya jirani kituo kilichozinduliwa na mwenge wa
uhuru.
Alisema
mpango wa uboreshaji wa kituo cha afya Levolosi kuwa hospitali ya jiji
umeshaanza ambapo fedha za mradi huo wa upanuzi na uwekaji wa vifaa tiba vya
kisasa zinatolewa na halmashauri ya jiji Arusha.
Akizungumzia
sekta ya elimu alisema jiji limeongeza vyumba vya madarasa na kujenga maabara
za kisasa kwenye skuli za sekondari za kata ikiwemo pia kuongeza madawati lengo
likiwa wanafunzi kupata elimu bora na kuondokana na tatizo la wanafunzi wanaochaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza kukosa vyumba vya madarasa.
Alisema
mpango huo umeshaanza kwenye skuli za Sonrenyi, Naura, Engutoto,Ngarenaro na
Felex Mrema na kwamba kwa sasa wamebakiza vyumba vya madarasa tisa tu hadi
mwisho mwa mwezi huu watakuwa wameshakamilisha madarasa hayo.
Aidha
alisema halmashauri ya jiji la Arusha imenunua vifaa vya ujenzi wa barabara
yakiwemo magari matatu,greda na kijiko vitakavyotumika katika ujenzi na
ukarabati wa barabara za jiji wakati pia magari yatasaidia uzoaji taka katika
maeneo jiji.
Alisema
jiji limejitahidi kuboresha madaraja na barabara zake na ipo mbioni kujenga
barabara ya Unga Ltd hadi Terati yenye urefu wa kilometa saba kwa kiwango cha
lami ambapo fedha zake zimepatikana na mradi huo kukamilika ndani ya miezi 14.
No comments:
Post a Comment