Na
Khamisuu Abdallah
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Dk. Islam Seif, amesema miongoni
mwa mikakati iliyowekwa na ofisi hiyo katika kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi ni kupanda miti pembezoni mwa bahari na juu Unguja na Pemba.
Alisema
hayo katika hafla ya upandaji miti katika kijiji cha Fuoni Kibondeni.
Nae
Mkuu wa wilaya ya magharibi Unguja, Ayoub Mohammed aliishauri jamii uwa mstari
wa mbele kuwadhibiti wanaoharibu mazingira na kuwahamasisha kupanda miti ili
uoto wa asili uendelee kuwepo.
Alisema
ili kuyahifadhi mazingira na kuyakinga maji ya bahari yasivamie vijiji ni vyema
kuwafichua watu hao na kuhakikisha rasilimali hiyo inalindwa kwa hali na mali.
Alisema
Zanzibar ni moja ya kisiwa kidogo
kilichozungukwa na bahari hivyo kuharibu mazingira kwa kuikata mikoko ni
kukaribisha athari za mabadiliko ya tabianchi.
Aliwaasa
wananchi kuwa makini na watu wanaoharibu mazingira kwa sababu za athari zake ni
kubwa kuliko faida.
Pia
alimtaka sheha wa shehia hiyo kutoa taarifa mapema ili hatua ziweze kuchukuliwa
na kuacha tabia ya kutosubiri kuharibiwa kwani waathirika wakuu ni wananchi.
Alisema
lengo ni kuhakikisha mazingira yanatuzwa na Zanzibar inarejea katika uhalisia
wake.
Ofisa
Misitu, Ali Ussi Basha, aliwataka wananchi wa shehia hiyo kuhifadhi mazingira
na kuendelea kupanda miti kwani ndio kimbilio kubwa la maisha ya mwanaadamu.
Jumla
ya mikoko na mikomafi 1000 imepandwa katika shehia ya Fuoni Kibondeni ili
kuhifadhi mazingira na kuyalinda maji ya bahari yasiingie katika maakaazi ya
watu.
No comments:
Post a Comment