Na Kauthar Abdalla
CHANZO
kikubwa cha migogoro kati ya waajiri na waajiriwa katika sekta binafsi ni
ukorofi kwa baadhi ya wawekezaji wazalendo.
Imeonekana
kuwa matatizo mengi yanayotokea katika sehemu za kazi ni maeneo ambayo
wawekezaji wake ni wazalendo na sio wageni kwa sababu wengi wanafuata sheria na
kanuni zilizowekwa.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Shangani, Kamishna wa kazi, Mashaka
Kubingwa Simba, alisema wawekezaji wazalendo huwa wanajali zaidi maslahi yao
badala ya maslahi ya wafanyakazi.
Alisema
kamisheni imekuwa ikipokea migogoro mbali mbali inayohusu wafanyakazi na wamekuwa
wakijitahidi kuitatua kwa mujibu wa sheria.
Alisema
ikishindikana inapelekwa mahakama kuu ambayo ina mamlaka zaidi ya kutoa uamuzi.
Aidha
alisema tatizo ambalo linawakumba wafanyakazi kujiingiza katika migogoro hiyo
ni uelewa mdogo zaidi wa sheria za kazi.
Aliwataka
wafanyakazi wa sekta binafsi ambao wanalipwa mshahara kima ambacho hakistahili kutoa
taarifa kamisheni ambayo kazi yake kubwa ni kusimamia sheria za kazi.
No comments:
Post a Comment