Na
Khamis Amani
Serikali imeshauriwa kuondoa muhali katika utatuzi wa changamoto mbali mbali
zinazozikabili jamii, ili ziishi kwa usalama na amani na ziweze kufanikisha
maendeleo ya familia zao.
Sheha
wa Shehia ya Kwahani wilaya ya mjini Unguja, Nassir Ali Kombo, aliyasema hayo
ofisini kwake wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, juu ya matatizo
yanayoikabili shehia hiyo.
Alisema
shehia hiyo ni moja kati ya shehia zilizokumbwa na wimbi la vijana wanaotumia
dawa hatari za kulevya, ambazo husababisha ongezoko la matukio ya kihalifu
ambayo ni hatari katika ustawi wa maendeleo ya maisha ya jamii.
Alisema,
japokuwa dawa za kulevya ni janga la taifa lakini serikali inapaswa kuondoa
muhuli kwa kuwadhibiti wale wote wanaoingiza dawa hizo, ili kuwanusuru vijana
ambao ndio nguvu kazi ya familia na taifa kwa ujumla.
Alisema
shehia ya Kwahani ni moja kati ya shehia zilizokumbwa na kadhia hiyo kutokana
na baadhi ya vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo, na kupelekea
kuwepo vitendo vya uhalifu.
Alisema,
wengi wa vijana wanaotumia dawa hizo wamekuwa wakikosa imani ndani na nje ya
familia zao kutokana na vitendo viovu wanavyovifanya.
Aliiomba
serikali kuondoa ukimya kwa kuwadhibiti wale wote wanaongiza dawa hizo kuliko
kuwakamata wauzaji wadogo.
Aidha
aliwaomba wananchi wote wa shehia hiyo kuweka mazingira yao katika hali ya
usafi hasa katika kipindi hiki cha mvua, ili kujikinga na maradhi ya miripuko
yakiwemo matumbo ya kuharisha.
No comments:
Post a Comment