Na Joseph Ngilisho, Arusha
RAIS Jakaya Kikwete,amesema
serikali imepiga hatua katika kuboresha zana za ulinzi za Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) na itaendelea kutenga fedha zaidi ili liweze kuwa na vifaa vya
kisasa zaidi.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya kilele cha kuhitinisha zoezi la medali ya
JWTZ,yaliyofanyika katika kijiji cha Nangururusu wilayani Monduli,ambapo
maadhimisho hayo yalienda sambamba na maonesho ya zoezi la kivita kwa kutumia
ndege, gari za deraya na jeshi la nchi kavu.
Alisema serikali imekuwa
ikitenga fedha kila mwaka kwa lengo la kuboresha maslahi ya wanajeshi pamoja na
kununulia vifaa vya kivita vinavyoendana na wakati ili jeshi hilo liendeleee
kuimarika zaidi na kuweza kukabiliana na chokochoko zozote zinazoweza
kujitokeza.
“Tunaendea kutenga fedha zaidi
ili kuboresha maslahi ya wanajeshi,tuna mikakatia mingi ikiwemo ya kuwapatia
nyumba, kujenga hospitali yao,tutaendea kufanya hivyo ili nitakapostaafu
niliache jeshi likiwa katika hali nzuri kidogo,” alisema.
Aidha alisema tangu kuanzishwa
kwa jeshi hilo Septemba1964, halijawahi kuacha misingi iliyoasisiwa na mwalimu
Julius Nyerere na kueleza kuwa litaendelea kusimamia misingi hiyo bila kukandamiza
wananchi.
Naye Waziri wa Ulinzi, Dk.
Hussen Mwinyi, alisema pamoja na serikali kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa zana
za kisasa,aliiomba iendelee kutenga fedha zaidi ili jeshi hilo likidhi mahitaji
ya kuwa na vifaa vya kisasa zaidi.
“Amri jeshi mkuu ana wajibu wa
kuangalia utendaji wa jeshi na vifaa vyake,hivyo tunaiomba serikali iendelee kutenga
fedha zaidi ili zisaidie kununulia vifaa vya kisasa,” alisema.
No comments:
Post a Comment