Na Khamisuu Abdallah
Wizara ya Afya imesema bado
inaendelea na utaratibu wa kugawa chakula kwa wagonjwa wanaolazwa katika hospitali
zake zote.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi ofisini kwake Mmnazimmoja,Katibu wa hosptali hiyo, Hassan Makame
Mcha, alisema utaratibu huo bado upo lakini kwa mujibu wa bajeti chakula hicho
kinatolewa kwa wagonjwa wasio na ndugu.
Aidha wagonjwa hao upatiwa mlo
wa mchana pekee lakini hali ya fedha inaporuhusu hupatiwa mlo kamili.
Hata hivyo, alisema hali ni
tofauti kwa hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu, ambao hupewa
chakula mara tatu.
“Kwa kweli tunaowaangalia sana
ni wale wagonjwa wa Kidongochekundu kutokana na hali zao, wale tunawapa mlo
kamili lakini kwa hospitali zetu mbili tumekuwa tukitoa mlo mmoja tu kwa wale wagonjwa ambao hawana ndugu,”
alisema.
Alisema tayari wameshaanda
bajeti ya chakula kwa wagonjwa na
ikipata ridhaa wataendelea kutoa mlo kamili kwa wagonjwa wote wanaolazwa katika
hospitali zao.
Aliwaomba wananchi kuendelea
kuzitumia hospitali zao kwani nia ya serikali ni kutoa matibabu bora kwa
wananchi.
No comments:
Post a Comment