Habari za Punde

Moto Wateketeza Nyumba ya Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar Mohammed Noshad Beitras jana.

Askari wa kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiwa katika harakati za kuzima moto uliozuka katika nyumba ya makaazi ya mfanyabiashara maaruf Zanzibar Mohammed Noshad ilioko betras Zanzibar jana jioni na kusababisha hasara kubwa katika tukio hilo la moto 

hii ni sehemu ya nyumba hiyo ikiteketea kwa moto na Askari wa Zimamoto wakiwa katika zoezi la kuuzima moto huo.








Mfanyabishara maaruf Zanzibar na aliwahi kuwa Mfadhili Mkuu wa timu ya Malindi Sp[ort Club, Ndg. Noshad Mohammed, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na janga hilo la moto lililoteketeza nyumba yake wakati wa majira ya jioni na kumsababishia hasara kubwa ya kupoteza mali.
Askari Jamii wa Shehia ya Betras akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuzima moto huo, akiwa katika eneo la tukio hilo betras.  

Sehemu ya nyumba hiyo ikiwa imeteketea kwa moto huo na kusababisha hasara kubwa

Ndugu na Jamaa wa Mfanyabiashara maarufu Zanzibar wakimfariji Ndg, Nashad baada ya ajali ya moto iliotokea nyumbani kweke na kuteketeza karibu vifaa mbalimbali viliokuwemo katika nyumba hiyo. 
Askari wa Usalama barabarani ikizuia magari kupita katika barabara hiyi kutowa nafasi kwa magario ya zimamoto kufanya kazi yake kuuzimas moto huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.