Na Zainab Anuwar
MWAKILISHI wa jimbo la
Kikwajuni, Mahamoud Mohamed Mussa, amewataka akina mama wa Saccoss ya Ishara
Njema, kuendelea kuimarisha umoja na ushirikiano ili waweze kujiletea maendeleo.
Aliyasema hayo Kilimani wilaya ya mjini Unguja, wakati akiwa katika
ziara ya kukitembelea Saccoss hiyo kwa lengo la kujua maemdeleo pamoja na
changamoto zinazowakabili wanachama.
Alisema ni vyema akina mama hao
kukiendeleza kwa ufanisi zaidi kikundi chao ili kiweze kuwasaidia katika mfumo
mzima wa maisha na kuachana na tegemezi.
Mwakilishi huyo alisaidia
shilingi 300,000 ili kusaidia maendeleo ya kikundi hicho.
Katibu wa Saccoss hiyo, Rukia
Omar , alisema lengo la kikundi hicho ni
kuwajengea uwezo akina mama kujiajiri na kupunguza utegemezi.
Hata hivyo, alisema
wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwmeo kutokuwa na soko la uhakika la kuuzia bidhaa
zao.
Nae Mwenyekiti wa Saccoss hiyo,
Hidaya Abdalah, alisema kutokuwa na mtaji wa kutosha ndio changamoto ya msingi
katika Saccoss hiyo.
No comments:
Post a Comment