Na Mwandishi wetu
Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
imetoa sarafu ya shilingi 500, ambayo itaanza kuingia kwenye mzunguko mwezi
Oktoba mwaka huu.
Mkurugenzi Huduma za Kibenki
kutoka Benki Kuu, Emmanuel Boaz, alisema hayo wakati akizungumza na waandishi
wa habari.
Alisema sarafu hiyo mpya ina
umbo la duara na michirizi pembezoni, rangi ya fedha na imetengenezwa kwa
madini ya chuma na nikeli.
Kwa mbele ina sura ya Rais wa
Kwanza wa Zanzibar, marehemu Sheikh
Abeid Amani Karume na kwa nyuma ina picha Nyati akiiwa mbugani.
Aidha ina alama ya usalama
iitwayo ‘latent image’ iliyopo upande wa nyuma
ambayo ni kivuli kilichojificha, kinachoonesha thamani ya sarafu ‘500’
au neno BOT inapogeuzwageuzwa.
Sarafu hiyo itatumika sambamba
na noti zilizopo sasa za shilingi 500 mpaka zitakapokwisha kwenye mzunguko.
Alisema sarafu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kwamba noti ya shilingi mia tano ndiyo inayotumika
zaidi kwenye manunuzi ya kawaida ya kila siku ya wananchi wengi kuliko noti
nyingine yoyote.
Hali hiyo husababisha noti hiyo kupita kwenye mikono ya watu wengi
katika kipindi mfupi na kuchakaa haraka.
Pia hukaa katika mzunguko kwa
muda mrefu bila kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili zibadilishwe
zinapokuwa zimefikia ukomo wake.
No comments:
Post a Comment