Na Aumbe Rashid
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Idara Maalum ya SMZ, Haji Omar Kheri, amewataka maofisa wa
Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kuwa na umoja,upendo na ushirikiano na kuyatumia vyema mafunzo waliyoyapata kwa
maslahi ya taifa.
Aliyasema hayo katika hafla
fupi ya ufungaji wa mafunzo ya kozi ya Platuni Kamanda,iliyofanyika kikosi cha
JKU Kama wilaya ya magharibi Unguja.
Aliwataka wahitimu wa mafunzo
hao kuzingatia majukumu yao, wanaporejea katika vituo vyao vya kazi.
Alisema ushirikiano ndio silaha
ya shinda changamoto zote zinazolikabili jeshi hilo.
Aliwaasa kutokuwa chanzo cha
migogoro kwa sababu inaweza kuchafua jeshi badala yake wafanye kazi kwa busara
zaidi.
Aliwataka wakuu wa idara za
jeshi hilo kusimamia vyema majukumu yao
na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Mkuu wa JKU, Kanali Soud Haji
Khatib, aliwapongeza wahitimu na wale wote waliosaidia kufanikisha mafunzo
hayo,wakiwemo walimu kutoka Jeshi la Kujenga Tafa (JKT) na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania(JWTZ).
Wahitimu katika risala yao
walisema wanakabiliwa na upungufu wa madarasa ya kusomea, nyumba za walimu na
vifaa vya kufundishia.
Mafunzo hayo yaliwashirikisha
askari 37 wakiwemo wanawake saba.
No comments:
Post a Comment