Na Mwandishi wetu
Askofu Mkuu wa Kanisla la Full
Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe, amesema kinachoendelea katika Bunge
Maalum la Katiba ni sawa na mchwa wanaotafuna fedha za Watanzania.
Alisema hayo jana katika
mahubiri yake ya Jumapili katika kanisa lake liliopo Mwengee, Dar es Salaam.
Aidha alisema kanisa lake
linaunga mkono tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu mchakato wa katiba.
Alisema kwamba Kanisa la FGBF
linaunga mkono tamko hilo kwa asilimia 200.
"Tamko hili limekuwa
likisomwa katika Makanisa ya Katoliki, KKKT, na mengineyo kuanzia Jumapili
iliyopita, na leo (jana) nitalisoma kwenu, neno kwa neon,” alisema.
Alisema wakati umepita wa
Wakristo kugawanywa, ili shetani atawale na kwamba tofauti zao wanazikweka pembeni
na kuunganishwa na msalaba.
“Jukwaa la Wakristo Tanzania
linawaunganisha wote wanaoamini juu ya msalaba - TEC, CPCT, CCT na SDA. Hivyo
kauli ya Jukwaa la Wakristo Tanzania, ni kauli ya FGBF, kwa sababu sisi tuko ndani
ya CPCT," Kakobe aliwaambia wafuasi wake.
Alisema rasimu ya pili ya Katiba ni waraka
halali na rasmi, na ndiyo mawazo ya Watanzania na kuongeza kuwa katiba ni ya
Wananchi na inahitaji maridhiano na sio ubabe.
Baada ya kusoma tamko la Jukwaa
la Wakristo Tanzania la Agosti 28, 2014, aliwauliza waumini,"anayeunga
mkono tamko hili asimame na kupunga mikono yake."
Ndipo wote kanisani waliposimama na kupunga
mikono yao huku wakishangiria kasha Kakobe akasema:"Pamoja na umuhimu wa
maombi, haitoshi tu kuomba; baada ya kufunga na kuomba, Esta alichukua hatua ya
kumwambia ukweli Mfalme. Pamoja na maombi, hatua ya Jukwaa la Wakristo Tanzania
kutoa sauti ya Kinabii kama hii, ni muhimu, ili mwenye masikio asikie."
Aliwataka waumini wake
wawapuuze watu wanaosema kufanya hivyo
ni kuchanganya dini na siasa.
“ Katiba siyo siasa, ni zaidi
ya siasa;siasa imo ndani ya katiba, lakini ndani ya katiba kuna mambo mengi pia
ambayo siyo siasa, kama vile dini, majeshi, mahakama, elimu, kilimo, ardhi, ufugaji,
haki za binadamu,” alisema.
No comments:
Post a Comment