Na Mwandishi wetu
Rais Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa
kukutana kwa mara ya pili wakuu wa vyama vya siasa vinavyounda Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD) kujaribu kukwamua mchakato wa katiba mpya.
Tayari Wenyeviti na Makatibu
Wakuu kutoka vyama hivyo wapo mjini Dodoma kwa ajili ya kuendeleza mazungumzo
hayo.
Kabla ya kukutana na Kikwete,
viongozi hao wa TCD jana walikutana faragha ili kupata taarifa ya kamati
iliyoundwa ambayo ilipewa jukumu la
kuchambua na kutoa ushauri juu ya mambo watakayokwenda nayo katika mkutano huo.
Kamati iliyopewa jukumu hilo,
inaongozwa na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia huku wajumbe wakiwa ni
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod
Slaa na Katubu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman
Kinana.
Kikao hicho kilikuwa na lengo
la kuweka msimamo wa pamoja kabla ya kukutana na Rais Kikwete.
Rais Kikwete anajaribu kukwamua
mchakato wa katiba mpya, baada ya wajumbe kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA) kususia bunge tokea mwezi Aprili, suala ambalo limezua mijadala mingi
kuhusu uwezekano wa kupatikana katiba mpya.
No comments:
Post a Comment