Na Mwandishi wetu
CHAMA cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA)
kimewapongeza wakazi wa mtaa wa Msigwa-Mbezi kwa Msuguri jijini Dar es Saaam
kwa kuchukua hatua za pamoja kulaani kitendo cha kulawiti kilichofanywa na mtu
mmoja alietajwa kwa jina la (40) kwa mtoto mwenye umri wa miaka mine.
Tukio hilo la ukatili
lililofanywa na mtuhumiwa hivi karibuni lilipelekea wakazi wapatao 23
kuandamana hadi ofisi za TAMWA zilizoko Sinza Mori wakiomba msaada wa kisheria
ili sheria iweze kuchukua mkondo wake baada ya kutoridhika na mwenendo wa kesi
inavyoendeshwa.
“Tumekuja TAMWA kulaani kitendo
cha ulawiti wa mtoto kilichofanywa na huyu baba mtu mzima. Sisi kama majirani
tumeona ni lazima tuchukue hatua na hatua yenyewe tulioichukua ni kuja hapa
kwenye shirika hili kuomba msaada kwani tunaamini linaweza kusaidia kupatikana
kwa haki,” alisema kwa uchungu mmoja wa wakaazi wa mtaa huo.
Mkazi huyo alisema wameamua
kuifuata taasisi ya hiyo baada ya kumuona mama wa mtoto huyo hajaridhika na
mwenendo wa kesi na hivyo kuiomba TAMWA iingilie kati ili serikali isikie sauti yao na kuhakikisha
inasaidia katika upatikanaji wa haki ya mtoto huyo.
Hatua ya wakazi hao inatokana
na elimu inayotolewa na TAMWA, kupinga vitendo ya ukatili na unyanyasaji wa
kijinsia hasa kupitia mradi wake wa Kujenga na kuimarisha usawa wa kijinsia na
kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto-(GEWE II).
TAMWA kupitia kituo chake cha usuluhishi
cha (CRC) kwa mwaka 2013 kilipokea jumla ya kesi 202 zinazohusu ukatili na
unyanyasaji kwa watoto ambapo wilaya ya Kinondoni ilipokea kesi 41, Temeke kesi
95 na wilaya ya Ilala ilikuwa na kesi 66.
No comments:
Post a Comment