Habari za Punde

Trafiki agongwa na kufa

Na Mwandishi wetu
 
ASKARI wa usalama barabarani, PW 2806 Koplo Riziki, amefariki dunia baada ya kugongwa na gari katika maeneo ya Mbagala rangi tatu.
 
Askari huyo aligongwa akiwa katika jitihada za kusimamisha daladala inayofanya safari zake kati Temeke na Mbagala Chalambe.

Baada ya kugongwa alipelekwa hospitali ya Temeke kwa matibabu na baadae kuhamishiwa Muhimbili, ambako alifariki dunia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.