Habari za Punde

Balozi Sefue awachimba mkwara watumishi wanaoshabikia siasa

Na Amina Omari, Tanga
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amewataka watendaji wa utumishi wa umma, kutojihusisha na ushabiki wa kisiasa ili kutekeleza majukumu yáo kwa ufanisi.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na watumishi wa sekretarieti ya mkoa na taasisi za serikali zilizopo mkoani Tanga.

Alisema nia ni kuhakikisha watendaji hao wanasimamia chaguzi zinazokuja kwa huru na haki.

Alisema taratibu za utumishi wa umma hazimruhusu mtumishi kujihusisha na ushabiki wa kisiasa wa aina yoyote.


Aliwata watumishi hao kufanyakazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuimarisha utendaji kazi serikalini.

Alisema ni lazima maadili ya utumishi wa umma yazingatiwe katika kutoa huduma kwa wananchi ili kuepusha migongano.

"Kuna malalamiko yanatokea kwenye huduma tunazotoa, wakati mwingine hadi majibu tunayotoa sio mazuri kwa wananchi hali hii inasababisha serikali tuonekane hatufanyi kazi,”alisema.

Alisemakwa sasa watakuwa wakichukua hatua kali kwa watendaji waoghushi madai ili kuitia hasara serikali.


Katibu tawala wa mkoa wa Tanga, Salum Chima, aliiomba serikali kuhakikisha wanawasilisha kwa muda fedha za miradi ya maendeleo ili kutekeleza kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.