Na Joseph Ngilisho, Arusha
UTATA umegubika kifo cha
mfanyabishara bilionea,Olais Metili (65) mkazi Uzunguni jijini Arusha,aliyefia
katika choo cha chumba alichokodi katika nyumba ya kulala wageni ya Diamond
Motel, ambapo familia imeshindwa kueleza undani wa tukio hilo.
Aidha katika hali isiyokuwa ya
kawaida wafanyabishara pamoja na majirani,waliususia msiba wa mfanyabiashara
huyo,huku idadi ndogo ya vijana na familia ndio waliojitokeza nyumbani kwa
marehemu.
Mdogo wa marehemu ambaye ndiyo
msemeji wa familia,Onesmo Metili, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani
tayari vyombo vya habari vinalifahamu.
“Mimi siwezi kuzungumzia suala
hilo kwani vyombo vyenu vya habari vimeandika amekufa kwa viagra sasa mnataka
niseme nini endeleeni kuamini hivyo,” alisema.
Mfanyabishara huyo alikutwa
amekufa katika nyumba hiyo ya kulala wageni mwishoni mwa wiki, akidaiwa kumeza
dawa ya kuongeza nguvu aina ya viagra baada ya kuingia na mwanamke kwa lengo la
kustarehe,ambaye hakufahamika mara moja.
Taarifa kutoka vyanzo vvya
habari katika nyumba hiyo, vimedai kwamba kwa muda mrefu marehemu amekuwa mteja
wao na pindi anapokuja hupiga simu na kuwataka wamwandalie chumba na pindi anapomaliza
kupumzika na mwenza wake hutoka na kurejea nyumbani kwake.
Siku ya tukio ilidaiwa kwamba
marehemu alifika akiwa ameongozana na mwanamke mmoja na alipofika alikodi
chumba na kuingia ndani,hata hivyo siku ya pili majira ya asubuhi,mhudumu mmoja
aliingia katika chumba hicho kwa lengo la kukifanyia usafi ndipo alipopigwa na
butwaa baada ya kukuta mwili wa mteja wao uko utupo ndani ya choo.
“Baada ya kuona mwili tulitoa
taarifa kwa uongozi ambao walipiga simu polisi,hatukujua kama kulikuwa na mtu
amekufa kwani ndani ya chumba kulikuwa hakuna mtu ila nilipojaribu kuingia chooni
ndipo nilikuta yupo chini amekufa,” kilisema chanzo hicho.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na ndugu wa merehemu,mwili wa mfanyabishara huyo utazikwa siku ya Ijumaa,kijijini
kwao eneo la Ilboru baada ya taratibu zote za kuuaga kukamilika.
No comments:
Post a Comment