Na Hafsa Golo
MAMLAKA ya Kuzuia Rushwa na
Uhujumu Uchumi Zanzibar, imesema itamchukulia hatua mfanyabiashara yeyote wa
vyakula na viburudishaji anaetoa huduma kwa wizara na taasisi za serikali,
ambae amekuwa akitoa risiti tupu kwa wanunuzi.
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,
Mussa Haji Ali alisema kufanya hivyo ni sawa na kuruhusu rushwa.
Alisema kitendo cha utoaji wa
risiti tupu kwa wanunuzi kutoka taasisi za serikali, ni miongoni mwa kuhujumu uchumi na rushwa na kurejesha nyuma juhudu za serikali za
kuwaletea wananchi maendelei.
Alisema katika uchunguzi wa
awali wamebaini kuwepo vitendo hivyo ndani ya taasisi za serikali,ambapo
wanunuzi hupewa risiti tupu na baadae hujaza kiwango cha fedha kinyume na hali
halisi ya manunuzi.
Alisema tayari ameshakaa pamoja na wafanyabishara
wanaotoa huduma hizo na kuwaelimisha madhara ya rushwa na kuwashauri kuacha
tabia hiyo.
“Baadhi ya wanunuzi wasio waaminifu wamekuwa
wakitumia fursa hiyo kujinufaisha bila ya kujali hasara serikali inayoipata,”
alisema.
Baadhi ya wafanyabishara
waliozungumza na gazeti hili walikiri kufanya biashara hiyo lakini baada ya
kupewa elimu hiyo, sasa wataacha.
No comments:
Post a Comment