Habari za Punde

ZANTEL Yazindua Kununua Umeme ZECO kwa EZYPESA Zanzibar Leo.



Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel Ndg. Pratap Ghose, akizungumza na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nisati Zanzibar Mhe. Ramadhan Abdalla Shaban wakati wa hafla ya kuzindua uuzaji wa Umeme kupitia Zantel na EzyPesa, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Grand Palace Malindi kusho aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Seif Rashid kwa sasa ni Waziri wa Afya Zanzibar.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel Ndg. Pratap Ghose, akizungumza na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nisati Zanzibar Mhe. Ramadhan Abdalla Shaban wakati wa hafla ya kuzindua uuzaji wa Umeme kupitia Zantel na EzyPesa, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Grand Palace Malindi kusho aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Seif Rashid kwa sasa ni Waziri wa Afya Zanzibar.  

MC Ndg. Kimeya akitowa utaratibu wa mwenendo wa hafla ya Uzinduzi wa Ununuzi wa Umeme kupitia Ezy Pesa mtandao wa Kampuni ya Zantel inatowa huduma hiyo kwa wateja wa ZECO Zanzibar, huduma hiyo inapatikana kupitia EzyPesa.  
Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Zantel wakifuatilia uzinduzi wa Ununuzi Umeme kupitia Kampuni yas Zantel kwa EzyPesa inayotolewa na Kampuni yao kwa wateja wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO.

Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Ndg.Hassan Mbarouk, akitowa maelezo kuhusiana na huduma ya kununua Umeme kupitia katika Mtandao wa Zantel wa EzyPesa, wakati wa uzinduzi huo na kuwataka wateja kutumia huduma hiyo inayotolewa kwa muda wa masaa 24, kwa kuuza Umeme na kuwataka kuwa wastaamilifu kwa usumbuvu utakaotokea wakati wa kipindi hichi cha mwazo mwa huduma hii.  

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu ya Zantel Tanzania Ndg. Pratap Ghose, akizungumza wakati wa uzinduzi huo na kueleza kampuni yake imejipanga katika kutowa huduma hiyo kwa muda wote wa masaa 24, huduma hiyo itapatikana na kuongeza huduma nyengine kwa wateja wake ili waweze kufaidika na Matunda ya kampuni ya Zantel katika kupata huduma bora za Mawasiliano.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel Ndg Pratap Ghose, akisisitiza jambo waki wa uzinduzi huo wa huduma ya ununuzi wa Umeme kupitia Ezy Pesa, huduma hiyo inayotolewa na Kamuni ya Zantel Tanzania unaweza kununua umeme wakati wowote na mahali popote Zanzibar utapata huduma hiyo.
Wakuu wa Idara za Serekani na Wananchi walioalikwa katika Uzinduzi wa huduma ya kununua Umeme kupitia Ezy Pesa uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace Malindi. 
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Zantel wakifuatilia uzinduzi huo wa kununua umeme kupitia EzyPesa. 

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mhe. Juma Duni Haji akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa ununuzi wa umeme kupitia EzyPesa

Waziri wa Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati Mhe Ramadhani Abdalla Shaban, akihutubia wakati kuzindua huduma ya Shrika la Umeme Zanzibar (ZECO)kununua umeme kupitia EzyPesa, inayotolewa na Kampuni ya Zantel. 
Wafanyakazi Shirika la Umeme na wa Zantel wakimsikiliza Waziri Shaban akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo ya ununuzi wa umeme kupitia EzyPesa.iliozinduliwa katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Grand Palace Malindi Zanzibar. 
            Wananchi waalikwa wakiwa katika ukumbi wa Grand Palace wakifuatilia hafla hiyo.


Waheshimiwa wa Kampuni ya Zantel wakifuatilia hafla hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel akitowa maelezo ya Huduma ya EzyPesa itakavyotowa huduma hiyo ya nunuzi wa umeme kupitia EzyPesa.
Waziri wa Ardhi Maakazi Maji na Nishati Mhe. Ramadhani Shaban, akimsikiliza  Mkurugenzi Fedha kupitia Mtandao wa ZYZPESA Ndg. Hashim Mukudi.akisoma tarakimu za umeme kupitia katika simu wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Granda Palace Malindi.
Waziri wa Ardhi Maakazi Maji na Nishati Mhe. Ramadhani Shaban, akizindua ununuzi wa Umeme wa Tukuza kupitia Mtandao wa Zantel wa EZYPESA, akiweka namba katika mita ya tukuza wakati wa uzinduzi huo, akisomewa namba hizo na Mkurugenzi Fedha kupitia Mtandao Ndg. Hashim Mukudi.imefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Zanzibar.
Waziri wa Ardhi Maakaazi Maji na Nishati Mhe. Ramadhani Shaban, akipiga makofi baada ya kuzindua ununuzi wa Umeme wa Tukuza kupitia Mtandao wa Zantel wa EZYPESA, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Zanzibar.
Waheshimiwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis, Mkurugenzi Mtendaji wa ZANTEL Ndg.Pratap Ghose, Waziri wa Ardhi Maakazi Nishati na Maji Mhe Ramadhan Abdalla Shaban, Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Ndg.Hassan Mbarouk, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Juma Duni Haji na Waziri wa Afya Mhe Rashid Seif Suleiman.
Mawaziri na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya Simu ya ZANTEL baada ya kuzindua ununuzi wa umeme kupiotia mtandao wa EZYPESA, uliozinduliwa na Waziri wa Ardhi Makaazi Nishati na Maji.Mhe. Ramadhani Abdalla Shabani  
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ZANTEL Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Zatel baada ya uzinduzi wa Kununua Umeme kupitia EZYPESA, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Grand Palace Malindi Zanzibar.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.