Habari za Punde

Ziara ya Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International

DSCN2320
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dk. Kassim Gharib Juma (kushoto) akibadilishana mawazo na Makamu wa Rais wa Shirika la Heifer International Steve Denne na Dk. Henry Njakoi, Mkurugenzi wa Shirika hilo nchini.
 
Steve Denne alitembelea Tanzania kwa mara kwanza wiki iliyopita kuona miradi inayoendeshwa na shirika hilo.
 
Katika ziara hiyo, Steve Denne alitembelea ofisi za mkoa wa Mbeya akifuatana na Mkurugenzi wa Heifer International Tanzania Dk Henry Njakoi, Meneja Mradi wa EADD Tanzania Bwana Mark Tsoxo, ambapo walikutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
 
Katika Mazungumzo yake na Mheshimiwa Abbas Kandoro, Bw Denne aliishukuru sana serekali ya Tanzania kwa mahusiano mazuri na ushirikiano mkubwa kwenye kutekeleza miradi ya shirika hilo nchini na hasa katika kuanzisha Mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD). Aliahidi kuwa shirika hilo kupitia mradi wa EADD na miradi mingine tarajiwa, litaendelea kuleta mabadiliko kwa kuwasaidia wafugaji wadogo kwenye mikoa wa Mbeya, Iringa na Njombe ili kuinua uchumi wao na kuwa na ufugaji wenye tija na endelevu.

 
Pamoja na miradi aliyoitembelea Steve Denne, mradi wa Uendelezaji Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) unaoanza Mkoani Mbeya wilaya ya Rungwe kijiji cha Kyimo ambapo aligawa mtamba kwa mfugaji wa kikundi cha Faraja kama dira ya shirika hilo ya “Toa Zawadi Pia” – Pass On The Gift.
 
Akiwa nchini, Makamu wa Rais wa shirika la Heifer International alikutana na wadau mbalimbali wa sekta ya maziwa nchini wakiwemo wasindikaji, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Jordan Rugimbana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Zanzibar ambapo alikutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dr. Kassim Gharib Juma.

1 comment:

  1. Dr. Kassim Gharib Juma. sikuamini namkumbuka akiwa bado kijana aliyekuwa akijipenda kwa kivazi na usafi sisi tuiwa wadogo katika ile miaka ya 90 tukimuona kama mfano wa kuigwa hasa aliporudi masomoni Uk nakumbuka kuna siku alitupa hadithi ya Mwanafunzi mwenziwao kutoka Israel aliyekuwa Uume wake haufanyi kazi lakini wanawake walikuwa wakijipanga kwa huduma zake sijuwi kama ilikuwa ni kweli au ndio masoga ya wazenj miaka ile kufurahisha na kucheka leo wapi

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.