Na Mwanajuma Mmanga
KITENGO cha Elimu ya Afya kimeandaa
mpango maaalum wa kutoa huduma za afya kwa watoto katika shehia ya Kandwi ili
kuwapunguzia masafa ya kufuata huduma za afya.
Hatua hiyo imekuja baada ya
wakaazi wa eneo hilo kufuata huduma hiyo katika kijiji cha Pwani Mchangani na
Chaani hali ambayo inawaletea usumbufu.
Abdulrahman Mussa, alisema
masafa ya kufuata huduma za afya ni marefua na yanasababisha baadhi ya wakati
watoto kukosa haki yao ya kupatiwa chanjo.
Alisema wakazi wa eneo hilo,
wamehamasika kupata huduma hizo lakini umbali wa vituo vya afya umekuwa kikwazo
hasa kwa watu wenye umri mkubwa.
Hata hivyo, waliiomba serikali
kuwajengea kituo cha afya ili tatizo hilo liondoke kabisa.
No comments:
Post a Comment