Na Khamisuu Abdallah
WAANDISHI wa habari nchini
wametakiwa kuibua masuala mbalimbali ya udhalilishaji wa kijinsia ili kuongeza
uelewa kwa jamii.
Akifungua mafunzo ya siku tatu
kwa waandishi wa habari yaliyofanyika Ofisi ya Watu Wenye Ulemavu Zanzibar
(ZANAB), Msimamizi wa vipindi vya redio kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania (TAMWA) kanda ya Dar es Salam, Judica Losai, alisema ikiwa waandishi
wa habari wataongeza uelewa na kuibua mambo mbalimbali ya udhalilishaji
itawawezesha watunga sheria kutoa sheria madhubuti ambayo itatoa haki kwa
wafanyaji wa vitendo hivyo.
Alisema ni vyema kwa wanahabari
kujikita zaidi katika kuelimisha jamii masuala ya udhalilishaji ili jamii iweze
kujitambua.
Aidha alisema lengo la mkutano
huo ni kuimarisha zaidi masuala ya udhalilishaji na kutoa muamko kwa jamii kuhusu
vitendo hivyo.
Kwa upande wake mwanachama wa chama
hicho kanda ya Zanzibar, Sophia Ngalapi, alisema ni vyema kwa waandishi hao
kuyafanyia kazi ipasavyo mafunzo watakayopewa na kuitumia vyema taaluma yao kwa
kuandika habari za udhalilishaji ili vitendo hivyo viweze kuondoka.
Nao wanahabari wakichangia mada,
walisema masuala ya udhalilishaji wa kijinsia yapo zaidi katika maskuli na vyuo
vya madrasa huku sheria ikiwa ndio changamoto kubwa ya kuzorotesha uendeshaji
wa kesi hizo.
Mafunzo hayo yameandaliwa na
TAMWA na kuwashirikisha wanahabari kutoka vyombo mbali mbali.
No comments:
Post a Comment