Na Salama Salim, ZJMMC
ZAIDI ya wanyama 21,000
wamepatiwa chanjo ya kuwakinga na maradhi ya kichaa cha mbwa katika maeneo
mbali mbali ya Zanzibar.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Maabara na Ufuatiliaji wa Magonjwa
ya Wanyama Zanzibar, katika Ofisi za Idara ya Huduma za Utabibu wa Mifugo, Dk.
Warid Abdalla Musa, alisema kampeni ya kuchanja wanyama hao inatekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la Kutetea Wanyama Duniani
na Serikali Zanzibar.
Alisema maradhi ya kichaa cha
mbwa yamekuwa yakiathiri mifugo kama vile mbuzi,ngo’mbe na paka na wakati
mwengine kusambulia binaadamu.
Maeneo yaliyoathirika zaidi na
maradhi hayo ni Ubago, Caheju na Koani kwa wilaya ya kati pamoja na Fuoni na
Chuini kwa upande wa wilaya ya magharibi.
Aidha alisema maeneo mengine
yalioathirika zaidi ni Donge na Zingwezingwe kwa upande wa mkoa wa kaskazini
Unguja.
Alisema maradhi hayo
yanasabishwa na virusi vinavyojuilikana kama NYSA vinavyoshambulia mishipa ya
fahamu, tezi za mate na viungo vya uzazi ambapo dalili zake ni kubadilika tabia
na mnyama kuwa mkali.
Alisema juhudi mbali mbali zinachukuliwa
ili kudhibiti maradhi hayo ikiwa ni pamoja na kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa
inayojuilikana kama ‘rabies vaccine’, ambayo hutolewa mara moja kwa mwaka
pamoja na kutoa elimu juu ya udhibiti wa maradhi hayo.
No comments:
Post a Comment