Baada ya Tamasha la
Fiesta kutangaza rasmi kuwa rapa na mshindi wa tuzo za Grammy, T.I wa Marekani
kuwa ndiye msanii mkubwa wa kimataifa atakayekuja kutoa burudani siku ya kilele
chake hapa Dar es Salaam, leo pia imetangazwa rasmi kuwa mavazi ya T.I ya
Hustle Gang, Akoo pamoja na Strivers Row nayo yatazinduliwa rasmi katika duka
la Pop Up Shop lililopo katika super market ya Dar Free Market siku ya tarehe
18-October, 2014.

Akizungumzia
uzinduzi huo wa mavazi ya T.I, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Grand Hustle
Records, Bwana Jason Geter ambayo ndio kampuni inayomsimamia msanii B.O.B na
mwanadada anayekuja kwa kasi Iggy Azalea, alisema anaamini soko la Tanzania na Afrika
kwa ujumla ni masoko makubwa kwa bidhaa zao.
‘Tuna matarajio
makubwa kuhusiana na kuleta bidhaa zetu nchini Tanzania, na tunatarajia sio tu
kuleta bidhaa zetu hapa nchini, bali kwenda mbali zaidi kwa kujifunza soko la
mitindo hapa nchini’ alisema Geter.
Duka la Pop Up
litafunguliwa kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saa tisa mchana ambapo wateja
watapata fursa ya kununua nguo halisia za Hustle Gang, Akoo na Strivers Row
Clothing, huku wamiliki wa maduka wakiweza kutazama bidhaa tofauti na kuagiza
oda zao.
Tamasha la Fiesta
ambalo linajulikana kama tamasha kubwa na lenye mafanikio zaidi kwa Afrika
Mashariki na Kati likiwa na wahudhuriaji wasiopungua 500,000 kwa mwaka huku
likijivunia wasanii wakubwa waliowahi kutoa burudani miaka ya nyuma kama Jay Z,
Ludacris, 50 Cent, Rick Ross na wengineo.
Mwaka huu kilele cha
tamasha la Serengeti Fiesta kitafanyika tarehe 18 mwezi wa kumi katika viwanja
ya Leaders jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment