Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake wakifuatana na mwenyeji wao Mkuu wa Kijiji cha
Uwekezaji wa Mji wa Chengmai Bwana Yang Si Tao wakielekea
ukumbi wa mkutano kwa mazungumzo.
Kulia ya Balozi Seif ni Mkurugenzi Mtendaji
wa ZIPA Nd. Salum Nassor Khamis, Mkurugenzi Mambo ya
Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo haji.
Mkuu wa Kijiji cha Maeneo huru ya uwekezaji katika Mji wa Chengmai aliyevaa
shati jeupe Bwana Yang Si Tao akimpatia maelezo Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kushoto
yake wakati ujumbe wa Zanzibar ulipoangalia maeneo hayo
ukiwa katika ziara ya siku 10 Jimboni Hainan
Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na
Ule mwenjeji wa
Hainan ukiongozwa na Gavana wa Jimbo hilo
Bwana Jian Dingzhi ukiendelea na mazungumzo yao ya uhusiano
hapo katika Hoteli ya Le Meriden Mjini Haikou.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi wa Kasha lililojaa
vyakula vya viungo { spices } Gavana wa Jimbo la Hainan
Bwana Jian, Dingzhi mara baada ya kumaliza mkutano wao
rasmi wa
ushirikiano.
Gavana wa Jimbo la Kisiwa cha Hainan Bwana Jian Dingzhi akibadilishana mawazo na
Mgeni wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.(Picha na Hassan Issa, OMPR China)
No comments:
Post a Comment