Na Othman Khamis OMPR China.
Uongozi wa Kisiwa cha Jimbo la Hainan Nchini
Jamuhuri ya Watu wa China iko tayari wataalamu na awekezaji wake kufungua milango ya uwekezaji katika Visiwa
vya Zanzibar katika miradi ya Kilimo, Utalii na Mazao ya
Baharini kwa lengo la kusaidi maendeleo ya Zanzibar.
Gavana wa Jimbo la Hainan Bwana Jian
Dingzhi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na
ujumbe wake ambao umenza ziara rasmi ya Kiserikali ya Siku
Kumi katika Jimbo hilo hapo Hoteli ya Le Meriden Mji Mkuu wa
Kisiwa hicho wa Haikou.
Bwana Jiang Dinmgzhi alimueleza Balozi Seif
kwamba Jimbo hilo ambalo ni Kisiwa kiliopo ncha ya
Kusini mwa China limekuwa na utajiri mkubwa wa wataalamu wa
Sekta hizo ambao unaweza kusaidia maendeleo na uchumi wa
Zanzibar.
Alisema Uongozi wakeutaandaa utaratibu na
mipango ya kusaidia kutoa taaluma ya kisasa kwa wavuvi
na wakulima wa Zanzibar ili wapate fursa ya
kuzalisha kitaalamu miradi yao hali itakayowaongezea kipato na
kupunguza umaskini.
Gavana Jian Dingzhi halifahamisha kwamba
hatua hiyo italenga kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria
uliopo kati ya Zanzibar na Hainan Visiwa vinavyolingana na
kufanana kimazingira.
Alielezea faraja yake kuona kwamba Kizazi
kipya cha jamii ya Wananchi wa Jamuhuri ya Watu wa China
kimekuwa kikijifunza uhusiano wa kidugu unaoendelea kuimarika
baina ya pande hizo mbili.
Gavana huyo wa Jimbo la Hainan aliwashauri
na kuwaomba wafanyabiashara wa Zanzibar kulitumia soko
la Hainan hasa lile la mazao ya Baharini katika kuendeleza
biashara zao.
Alisema Hainan imekuwa mzalishaji mkubwa wa
mazao ya Baharini yanayokadiriwa kufikia Tani 50,000
ndani ha mwaka huu wa 2014.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Sekta za Kilimo,
Utalii na Mazao ya Baharini zimekuwa zikitoa
mchango kuongeza mapato ya Taifa.
Balozi Seif alimueleza Gavana Jian Dingzhi
kwamba ziara ya Ujumbe wake ndani ya Jimbo la Hainan itatoa
fursa ya kujifunza maendeleo yaliyopatikana
ambayo yameliwezesha Jimbo hilo kupata ufanisi
mpana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
aliushauri Uongozi wa shirika la Ndege la Hainan kuanzisha safari
za moja kwa moja za usafiri wa anga kati ya Visiwa hivyo kwa
lengo la kupanua wigo wa biashara hasa utalii.
Alisema uamuzi huo endapo utafikiwa unaweza
kutoa nafasi kwa wawekezaji wa Hainan kuhamasika na hatiame
kuamua kuwekeza miradi yao ya kiuchumi katika Visiwa vya
Zanzibar.
“ Ziara yangu hii pamoja na mambo mengine
ya ushirikiano na uhusiano kati ya Zanzibar na Hainan
lakini pia imelenga kushawishi wafanyabiashara na wawekezaji wa
Hainan kuwekeza vitega uchumi vyao Zanzibar “.Alisema
Balozi Seif.
Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake walitembelea meneo huru
ya uwekezaji pamoja na kuangalia uzalishaji katika
kiwanda cha usindikaji Samaki kwenye mji wa Kisiwa cha Haina,
Haikou.
Akizungumza na wawakilishi wa Kiwanda hicho
na ule wa Maeneo huru ya uwekezaji wakiongozwa na Meya wa
Mji waChengmai Bwana Zhaomin Ji , Balozi Seif aliwapongeza
Wananchi wa Hainan kwa hatua kubwa waliyofikia katika
kuimarisha maendeleo yao.
Balozi Seif maendeleo hayo yanatoa nafasi
kwa Zanzibar kujifunza kupitia ziara za mara kwa
mara za viongozi
na watendaji wake.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imeanzisha maeneo huru ya uwekezaji pamoja na mfumo wa
Bandari huru ya kiuchumi ili kuimarisha maendeleo yake
lakini bado miundombinu katika maeneo hayo yangali
duni.
Naye Msaidizi wa Meya wa Mji wa Chengmai
ambae pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Kamati ya Chama ya Mji huo
Bwana Sitao Yang alisema Hainan ni miongoni mwa Majimbo
yenye rasilmali kubwa ya kiuchumi ikitanguliwa na Taiwan.
Alisema uchumi wa Jimbo la Hainan umekuwa
na kufikia uwekezaji wa Yuan Bilioni 20 mwaka huu
kutokana na kuimarika kwa miundo mbinu yake inayotoa fursa katika
uwekezaji wa sekta ya Utalii.
Bwana Sitao alimuhakikishia Balozi Seif
kwamba juhudi zitaongezwa katika kuona uhusiano wa kidugu naendelea kuimarika kati ya Zanzibar na Hainan kwa
kuweka ubia katika miradi ya kiuchumi na maendeleo.
Wakati wa Jioni Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar na Ujumbe wake walijumuika pamoja na wajumbe wa
Mkutano wa Tato wa Ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye
chakula cha jionikilichoandaliwa na Gavana wa Hainan
Bwana Jian Dingzhi hapo kwenye Hoteli ya Le Meriden Mjini
Haoku.
Kuna haja gani ya yeye kwenda huko. Juzi tu Raisi Kikwete karudi kutuombea na sisi misaada. Kwanini isiwe imetosha, vipi wachina watakuamini usemayo wakati Zanzibar haitambuliki kimataifa. Au na hii ni regesha bwege ya kuiba pesa kama ile ziara yako yako Seattle, Washington.!!!!!!!
ReplyDelete