Habari za Punde

Maali Seif Atembelea Majeruhi wa Ajali Kitope.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akimjuilia hali mzee Shihab Ahmed ambaye ni miongoni mwa majeruhi wa ajali ya gari iliyotokea eneo la Kitope, mkoa wa Kaskazini Unguja walipokuwa wakielekea kwenye mkutano wa hadhara wa CUF. Kati kati ni daktari Abdulaziz Mohammed wa hospitali ya Mnazimmoja mjini Zanzibar. (Picha na Salmin  Said, OMKR)

Na Khamis Haji OMKR.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewatembelea majeruhi wa ajali ya gari iliyotokea Jumapili iliyopita katika eneo la daraja la Kitope, mkoa wa Kaskazini Unguja.

Majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya Mnazimmoja walipata ajali hiyo walipokuwa wakielekea Fukuchani, Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja kuhudhruia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho na kuhutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CUF Taifa, Mhe. Juma Duni Haji.

Akitoa maelezo juu ya maendeleo ya afya za majeruhi hao kwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Daktari Abdulaziz Ahmed amesema majeruhi wote afya zao ni nzuri na wanaendelea kupata matibabu bila ya matatizo yoyote.

Naye Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatembela majeruhi hao, amesema amepata faraja kubwa baada ya kuelezwa na madaktari dhamana kuwa majeruhi hao wote wanaendelea vizuri na matibabu na afya zao ni nzuri.

Hata hivyo ametoa wito kwa maderea wote wakiwemo wale wanaoendesha magari ya mizigo kama vile ya mchanga kuchukua tahadhari kubwa wanapokuwa barabarani ili kuepusha ajali zisitokee.

Amesema babara inatumiwa na watu wengi, hivyo ni jukumu la madereva kufuata sheria za barabarani kikamilifu, ili kuepusha ajali ambazo matokeo yake ni kusababisha maisha ya watu kupotea na wengine kupata ulemavu.  

Ajali hiyo iliyotokea katika daraja la Kitope ilitokea baada ya gari aina ya Fuso iliyokuwa limebeba sheheana ya mchanga ilipoigonga gari aina ya Hiace walimokuwemo majeruhi hao pamoja na abiria wengine ambao jumla walikuwa 12.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.