Habari za Punde

Mhe.Spika Anne Makinda Ashiriki Mkutano wa IPU UMOJA WA MATAIFA

                              Mhe. Spika akibadilisha mawazo na   viongozi wa IPU
 Mhe. Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda ( Mb) akifuatilia majadiliano yaMkutano wa  Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, Mkutano  huu wa siku mbili unafanyika hapa Umoja wa Mataifa
                                        Mhe. Spika akisalimiana na  Spika wa Bunge la India
                              Mhe, Spika  Anne Makinda akisalimia kwa furaha na  Spika wa Bunge la Uruguay


Na MwandishiMaalum, New York
Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge, jana jumatatu,imeanza mkutano wake wa pili na wa siku mbili unaofanyika hapa Umoja wa Mataifa. 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda (Mb)  ni miongoni mwa washiriki wa Kamati hiyo ya Maandalizi ukiwahusisha maspika kadhaa kutoka mabunge mbalimbali duniani. 

Katika mkutano huo wa siku mbili ambao umeandaliwa na Inter-Parliamentary Union (IPU),wajumbe wa kamati hiyo wanajadili mapendekezo ya Maudhui na Tamko la Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge unaotarajiwa kufanyika mwaka 2015.  Aidha wajumbe hao wanatarajiwa pia katika siku mbili hizi kutoa uamuzi wapi kutakakofanyikia mkutano huo. 

Maudhui na Tamko la mkutano huo wa Nne pamoja na  mambo mengine yanatarajiwa kuwa yatazingatia vipaumbele au mambo muhimu naya msingi ya mahitaji ya mwanadamu katika dunia ya sasa.  Mambo ambayo pia ni ajenda muhimu katika Umoja wa Mataifa 

Baadhi ya mambo hayo na ambayo wajumbe wa kamati ya Maandalizi wanayapitia ni pamoja na,tathimini ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDGs),Mapokeo ya Agenda Mpya za Maendeleo Endelevu baada ya 2015, na maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. 

Katika siku ya kwanza ya mkutano wao wajumbe wamesikiliza thathmini ya utekelezaji wa MDGs, kutathmini yaliyotolewa na Spika wa Bunge la Iceland ambaye ameainisha mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa malengo hayo ambayo yanafikia ukingoni mwakani. 

Pamoja na kusikiliza tathimini ya  MDGs,   Maspika hao pia wamepata fursa ya kubadilishana mawazo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja anayehusikana SDGs, Bi Amina Mohammed ambaye ametoa muhtasari wa ajenda na malengo mapya ya  SDGs baadaya  2015. 
Katika maelezo yake  Bi Amina ametilia mkazo ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa,

Serikali na nafasi ya Mabunge katika utekelezaji wa SDGs huku akisisitiza kwamba changamoto kubwa na muhimu katika utekelezaj iwa SDGs hizo ni suala na uwezeshaji wa raslimali fedha, suala ambalo amesema linahitaji ushirikiano wa pamoja katika kulipatia muelekeo wake.

Aidha amewaeleza wajumbe wa Kamati kuwa Maspika na wabunge katika kila  Bunge duniani kote wanapaswa kuwa weledi na wenye ufahamu mkubwa kuhusu SDGs yenye ajenda 17 na malengo 169 kwa kuwa wao ndio wawakilishi halisi wa wananchi waliowachagua.

Akasisitiza kuwa wabunge wanapaswa kushirikiana kikamilifu na serikali katika utekelezaji wa SDGs na huku au kubemba ujumbe wa mambo muhimu na ya msingi kwa mahitaji masuala ambayo ni muhimu kwa maisha ya Maspika kadhaa ambao ni wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Dunia wa Maspika wa Mabunge utakaofanyika mwakani.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.