Habari za Punde

Moja ya Nyumba katika Mji Mkongwe Yaanguka leo asubuh.Zanzibar

Moja ya Jengo katika Mji Mkongwe linalomilikiwa na Ndg. Rashid Abass Imram, limeaguka leo asubuhi kutokana uchakavu wake na baadhi ya wananchi wanaokaa jirani na jengo hilo wamesema jengo hilo lilikuwa na ufa kwa muda mrefu bila kufanyiwa ukarabati na mwenye nyumba hiyo, kutokana mvua zinazonyesha hivi sasa katika visiwa vya zanzibar zimesababisha jengo hilo kupata maji nakuta zake na kuanguka.

Mashuhuda wa ajali hiyo wasema jengo hilo limepata ajali hiyo wakati wa saa moja asubuhi leo ikitokea ajali hiyo kulikuwa hakuna watu wakiwa wamekaa baraza eneo hilo hutumika kwa wakaazi wa sokomuhoga kukaa jirani na maskani ya jozcorner, Katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa ila kunasemekana kuna mtoto hakuonekana mpaka sasa wanashaka kuwa labda amefunika na kivushi hicho Harakati za Kikosi cha Uokozi cha Zimamoto Zanzibar wakiendelea na kuvukua kivusi hicho kuona kama kuna mtu amefukiwa na kifusi cha nyumba hiyo
Askari swa kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiwa kastika jitihada za kuondoa kifusi kuangaliwa kama kuna mtu aliyefunikwa na kifusi cha jengo hilo lilioko jirani na maskani ya Joz Conern sokomumogo.  
Waokoaji wakiwa katika harakati za kuondoa kifusi kuona kama kuna mtu aliyefunikwa na kifusi hicho baada ya kuanguka kwa jengo hilo ambalo lilikuwa halina wakaazi katika jengo hilo lenye gorofa tatu kwa sasa lilikuwa halikai wati ila kulikuwa na wafanyabiashara wa vinyago milango ya chini ya jengo hilo wakati ikitokea ajali hiyo mweye duka hilo hakuwekwe katika biaashara yake.




3 comments:

  1. historia ndo inaondoka hiyo hao watalii sijui watakuja kuangalia nini tena

    ReplyDelete
  2. usalama wa raia ni bora kuliko kuwa na majumba mabovu yenye kuhatarisha maisha ya wananchi ili yawe vivutio kwa watalii , tuna mambo mengine watalii watakuja kuona ktk nchi yetu ( au sio nchi vile ni mkoa?)

    ReplyDelete
  3. Watakuja kutizama wamasai Kiwengwa.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.