Habari za Punde

Ubalozi wa Tanzania nchini China waandaa Tafrija maalum kwa ujumbe wa Zanzibar

  Ujumbe wa Zanzibar uliokuwa nchini China kwa ziara ya Kiserikali ukipata mlo kwenye Tafrija  maalum waliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Nchini China.

Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. Said Hassan Said, Meya wa Manispaa ya Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib, Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban,Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Mh. Ussi Jecha Simai.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwa pamoja na Mke wa Balozi wa Tanzania Nchini China Mama Mary  Antony  Tairo pamoja na Afisa wa Ubalozi huo Nd. Kitokezi Juma Kitokezi wakiwa kwenye Tafrija iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Nchini China kwa ujumbe wa Zanzibar.
  Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya China        { BCEG } Mhandisi  Tiger Nzu akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wake ulipofanya ziara ya kutembelea uwanja wa Kimataifa wa Beijing Nchini China ambao umejengwa na Kampuni hiyo ya BCEG.

Nyuma ya Mhandisi Tiger Nzu  ni Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk, kati kati ya Balozi Seif na Mh. Said ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo, kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban na nyhuma yake ni Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Mh. Ussi Jecha Simai.
Balozi Seif akizungumza mara baada ya Tafrija iliyoandaliwa na Kampuni ya Ujenzi ya BCEG kwa ajili ya Ujumbe wake baada ya kumaliza kuitembelea uwanja wa ndege wa Beijing Nchini China.
Mbele ya Balozi Seif aliyevaa miwani na kukaa ni Naibu  Meneja wa Kampuni ya BCEG Bwana Dinng Chuanbo.

Picha na Hassan Issa , Beijing China.

1 comment:

  1. AG wetu hapo kapata mamboye, nasikia anapenda sana mpunyenye. Jikate Baba, ukatumalize Dodoma.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.