Na Hafsa Golo
Msikiti mkubwa unaojengwa na
Mfalme Qaboos wa Oman ambao una uwezo wa
kusaliwa na waumini zaidi ya 1,000 kwa
wakati mmoja, umefikia hatua nzuri ya ujenzi wake na na unatarajiwa kukamilika
mwaka 2016.
Hayo yamebainika wakati Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe. Ali Juma Shamuhuna, alipotembelea msikiti
huo kuangalia ujenzi unavyoendelea.
Meneja wa mradi wa ujenzi wa msikiti
huo, Mhandisi, Ahmed Khalfan Al-shukaili, alisema ujenzi
ulitarajiwa kukamilika mwaka ujao lakini haitowezekana kwa sababu ya kuchelewa baadhi ya vifaa.
Aidha alisema msikiti huo
unajengwa kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha unadumu kwa zaidi ya karne moja
bila kujitokeza athari.
“Msikiti tunaojenga utapendeza kama Mfame
alivyoagiza na Mwenyezi Mungu akijaalia utadumu milele bila kujotokeza
hitilafu,” alisema.
Naye Waziri Shamuhuna, alisema msikiti huo pia utakuwa na chuo cha kiislamu
kitakaochukua zaidi ya wanafunzi 100 kwa wakati mmoja.
Mkuu wa Chuo cha Kiislamu
Mazizini, Dk. Muhyddin Ahmad (Maalim Siasa), alisema iwapo chuo hicho
kitaanzishwa wanafunzi watafundishwa na walimu wazalendo.
Alisema wapo walimu wanne wenye
shahada ya uzamivu (Phd) na 21 shahada ya uzamili na kwamba walimu 18 wako
masomoni nje ya nchi wakisomesha shahada ya uzamili na uzamivu.

Andika vizuri. Huo msikiti unajengwa wapi?
ReplyDeleteHawa waandishi wa siku hizi ndio hivo hawaelezi yakaeleweka story hajakamilika. Msikiti unajengwa wapi ?
ReplyDeleteHuo msikiti unajengwa mazizini opposite na kituo cha polisi sawa
ReplyDelete