Habari za Punde

Msikiti wa Sogea unahitajia msaada wako kupandisha Ghorofa




Msikiti wa Sogea uliopo jirani na Branchi ya Sogea unawaomba Waislamu popote mlipo katika ulimwengu huu wa Arrahmaan kuungana nao tena katika kuwapatia msaada ili uweze kuweka jamvi (Zege) la ghorofa ya kwanza (concrete ceiling).

Pesa inayohitajika kwa ajili ya jamvi ni zaidi ya shilingi Milioni tatu.

Pia tungeliomba msaada wa kuendelea na ujenzi mpaka umalizike Msikiti wote kiasi ambacho ni zaidi ya shilingi Milioni kumi.

Sababu ya kuamua kupanua msikiti ni kwamba kila Ijumaa watu hujaa hadi kuswali nje ambako ni barabara kuu kwani ni hatari kwa magari na wapita njia. Tunamuomba Allaah Subhaanahu Wata'ala atunusuru na ajali.

Tafadhali tunakuomba ujitahidi kwa uwezo wako wote wewe mwenyewe kwanza na uwaombe Waislamu wengine ili tuweze kuumaliza kwa muda mfupi kabisa.


Allaah Subhaanahu Wata'ala anatukumbusha katika Qur'aan "Na kheri yoyote mtakayoitanguliza kwa ajili yenu basi mtaikuta mbele ya Allaah itakuwa kheri kubwa na (yenye) ujira mkubwa" Suuratul Muzammil

Kwa maelezo zaidi na vipi kuwasilisha sadaka yako, wasiliana na Imaam wa Msikiti wa Sogea Sheikh Suleiman Bin Daaud +255 777 460 056
 


Tafadhali mpelekee ujumbe huu kila mtu, mkono kwa mkono mpaka Peponi.

Baaraka Llaahu fiykum

1 comment:

  1. Shime waislaam tujitahidini kutengeneza akhera zetu. Ila Nina wazo kidogo kwa mujibu Wa eneo ulipo msikiti nahisi ni busara pia kuusogeza mbele huu msikiti kwani upon karibu mno name barabara kuu. Naamini utanuzi wowote Wa Barbara hii huenda utahusisha uvunjaji Wa sehemu ya msikiti kwa hi yo ni vyema tukalifikiria mapema hili kujenga ghorofa ni jambo jema sana Mimi nashauri hata tukiweka ghorofa 3 au 4 ni aula mila pia tufikirie njia za kuusogeza mbele kidogo.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.