Habari za Punde

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdurahaman Kinana Wilaya ya Kati.Unguja.

Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg. Sauda Mpambalyoto, akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchuguzi ya Chama cha Mapinduzi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdurahaman Omar Kinana alipoaza ziara ya Wilaya hiyo ya Kati Unguja kuazia Afisi ya CCM ya Wilaya ya Kati Dunga.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdurahaman Kinana akizungumza na Viongozi wa CCM katika viwanja vya Afisi hizo huko Dunga Wilaya ya Kati Unguja baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji ya Wilaya hiyo, kabla ya kuaza ziara yake katika Wilaya hiyo Kichama.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdurahaman Kinana kizungumza baada ya kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na uimarishaji wa miradi ya Wananchi na kuimarisha Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdurahaman Kinana kizungumza baada ya kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na uimarishaji wa miradi ya Wananchi na kuimarisha Chama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdurahaman Kinana akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Ndg, Vuai Mwinyi, kuelekea katika Jengo jipya ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja.linalojengwa na Serekali kwa ajili ya Ofisi ya Wilaya lilioko Dunga Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Ndg Vuai Mwinyi akitowa maelezo ya Ujenzi wa Jengo la Kisasa la Ofisi ya Wilaya ya Kati Unguja linalojengwa katika Eneo la Dunga Unguja.
Katibu Mkuu akijenga taifa katika ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja akiwa katika ziara yake Unguja
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdurahaman Kinana akishiriki katika ujenzi wa taifa katika jengo la Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja akimwaga zege katika moja ya linta za jengo hilo huko dunga Unguja.
Waandishi wakiwa katika harakati za kuwahi kupata picha bora kwa ajili ya vyombo vyao vya habari wakati wakiwa katika ziara ya Ndg. Kinana Dunga Unguja
























No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.