Habari za Punde

Dk Shein mgeni rasmi siku ya kilele cha mazoezi ya viungo kitaifa

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa akiwa na Viongozi wengine yaliyoanzia  katika Uwanja wa Tumbaku hadi Uwanja wa Amaan Studium leo asubuhi ambapo yamejumuisha Vikundi mbali mbali vya Unguja na Pemba,[Picha na Ikulu.]
 Miongoni mwa vikundi vilivyoshiriki katika matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa ni kikundi cha KVZ Fitness Group kikiwa katika hali ya ukakamavu na nidhamu ya juu wakipita katika barabara Kariakoo kuelekea Komba wapya ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliyaongoza  matembezi hayo leo asubuhi ,[Picha na Ikulu.]

 Kundi la Mazoezi Zoni C wakiwa na bango lao linalosomeka  "Siku ya Mazoezi Kitaifa  01Jan 2015 Mazoezi ni Tiba Mbadala",kama wanavyoonekanwa wakiwa katika matembezi ya Siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa leo yaliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipunga mkono kama ishara ya kuyapokea matembezi ya Vijana wa Vikundi vya mazoezi katika kilele cha Siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo asubuhi (kushoto kwa Rais)  Mwenyekiti wa Zabesa Mohamed Suleiman Zidi, . [Picha na Ikulu.]

 Baadhi ya Wafanyakazi wa Vikosi vya Ulinzi wakiwa katika jukwaa wakiangalia harakati za mazoezi yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium wakati wa Siku ya KIlele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]

 Vijana wa makundi mbali mbali wakiwa katika mazoezi ya jumla leo katika Kilele cha siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]
 Vijana wa makundi mbali mbali wakiwa katika mazoezi ya jumla leo katika Kilele cha siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Studium akiwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika Kilele cha Siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Cheti cha Heshima kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha  Zabesa Mohamed Suleiman Zidi, katika Kilele cha Siku ya Mazoezi ya Viungo Kitaifa leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi cheti Ahmed Ali Zoni A yenye maeneo ya Maisra-Ngazi mia katika siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa katika hafla iliyofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimakabidhi cheti Sande Kichumvi wa Kikundi cha mazoezi cha wakali kutoka Dar es Salaam kwa ushiriki wao  katika siku ya Kilele cha Mazoezi ya Viungo Kitaifa katika hafla iliyofanyika leo uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.