Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg Abdulrahaman Omar Kinana akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A katika viwanja vya Nungwi baada ya kumaliza ziara yake katika Wilaya hiyo kuimarisha Chama na kuangalia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katibu Mkuu Ndg Kinana akisisitija jambo wakati akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika viwanja vya Mpira Nungwi baada ya kumaliza ziara yake katika Wilaya ya Kaskazini A Unguja
Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini Unguja wakiwa katika viwanja vya mkutano wa hadhara katika viwanja vya mpira nungwi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mbunge wa Viti Maalum Mhe Kidawa akihutubia katika mkutano huo na kuwataka Wananchi wa Nungwi kupiga kura ya Ndio kuipitisha Katiba mpya iliopendekezwa na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba. Akiwa na Katiba iliopendekezwa na kuwasomea Vifungu vya Katiba hiyo.
Viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya mpira Nungwi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini A Unguja Ndg, Ali Makame akihutubia katika mkutano huo wa hadhara katika viwanja vya mpira Nungwi Unguja.
Viongozi wa meza Kuu wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja, akihutubia wakati wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Kinana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mpira Nungwi Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Katibu wa Halmashauri Kuu Uenezi na Itikadi Ndg. Nape Mnauye akihutubia katika mkutano huo na kutowa elimu kwa Wananchi wa Nungwi, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mpira nungwi Unguja.
Ndg Nape akiwa na msisitizo wakati akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja katika viwanja vya mpira nungwi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, akihutubia katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mpira nungwi, na kutowa elimu kwa wananchi wa nungwi kwa kufafanua baadhi ya vifungu vya Katiba iliopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba vilivyotowa fursa kwa Zanzibar, na kuwata kupiga kura ya ndio wakati wa kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika mwezi wa April2015.
Wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A wakiwa katika viwanja vya mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mpira nungwi, baada ya kumaliza kwa ziara yac siku moja Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana na kesho kuendelea na ziara yake katika Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kuskazini Unguja.
Sura zile zile. Ccm watu kibaoooo.
ReplyDelete