Habari za Punde

Mkutano wa Hadhara Viwanja vya Kwabinti Hamrani Jangombe

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Ndg, Abrahaman Kinana akiwasili katika viwanja vya Mkutano Jangombe kwa Bint Hamrani kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja hicho baada ya ziara yake Mkoa wa Mjini Unguja na kuwahutubia WanaCCM wa Mkoa huo.
Viongozi wa Chama wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana alipowasili katika viwanja vya mkutano Jangombe kwa Ninti Hamrani Unguja.
Wabunge na Wawakilishi wa CCM wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM alipowasili katika viwanja vya mkutano Kwabinti Hamrani Unguja.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abrahaman Kinana akiwahutubia Wananchi na WanaCCM katika mkutano wa hadhara baada ya kumaliza ziara yake katika Mkoa wa Kichama wa Mjini, mkutano huo umefanyika katika viwanja vya kwabinti Hamrani Unguja.  
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abrahaman Kinana akisisitiza jambo wakati akiwahutubia WanaCCM, katika viwanja vya Kwabinti Hamrani Jangombe, akihutubia baada ya kumaliza ziara yake katika Mkoa wa Kichama wa Mjini.  
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika viwanja vya kwabintiHamran, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abrahaman Kinana, 
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi wakati akiwa jukwaani akiwahutubia katika viwanja vya Kwabinti Hamrani Jangombe akiwa katika ziara yake Zanzibar kwa kuimarisha Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg Vuai Ali Vuai, akihutubia mkutano huo na kusoma baadhi ya vipengele vya Katiba Iliyopendekezwa na Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba, inayotarajiwa kupigia Kura ya Maoni mwenzi April 2015.  
Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM Ndg. Nape Mnauye, akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kwabint Hamrani Jangombe, 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Ndg. Borafya Silima akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Mkoa wa Mjini baada ya Katibu Mkuu wa CCM kumaliza ziara yake katika Mkoa huo.na kuendelea na ziara yake katika mikoa mengine ya Kichama.
Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Mhe. Shamsi Vuai Nahodha akihutubia katika mkutano huo na kuchambua baadhi ya Vipengele vya Katiba kwa Wananchi ili kuielewa na kuipigia Kura ya ndio siku ikifika mwenzi April 2015.
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano wa hadhara katika viwanja vya kwabint Hamrani Jangombe.Unguja.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Mhe, Hamza Hassan, akihutubia katika mkutano huo wa hadhara kwa Wananchi wa Mkao wa Mjini. 






No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.