Habari za Punde

Mshitakiwa wa unga apigwa risasi akikimbia mahakamani

Na Fatuma Kitima,DAR ES SALAAM
MSHITAKIWA Abdul Koroma kutoka Sierra Leone ambaye alitumiwa kwa kosa la dawa ya kulevya amejaribu kutoroka kwa kuruka uzio wa mahaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza na wengine.

Katika juhudi za kumdhibiti alipata majeraha baada ya kufyatuliwa risasi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kamishna polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema mtuhumiwa alikuwepo mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Alisema hadi sasa hawajui kwanini alikuwa anataka kutoroka hivyo watamuhoji na kujua chanzo cha kufanya hivyo.
Aidha aliwaonya watu watakaofanya vurugu katika mkesha wa mwaka mpya wa 2015.

Alisema polisi wamejipanga kikamilifu kupambana na watu watakaofanya vurugu kwa kuhakikisha sherehe hiyo inasherekewa kwa amani na utulivu.
Alisema katika suala zima la ulinzi jeshi la polisi litashirikiana na kampuni binafsi za ulinzi ili kufanya kazi kwa ufanisi na kushughilikia wale wote watakaosherekea kwa fujo.

 Aidha alieleza kuwa kila barabara wameweka ulinzi  ikiwemo barabara ya viwanja vya kimataifa vya Mwalimu Nyerere.
Alianisha kuwa kuna baadhi ya watu waliomba vibali vya kupiga baruti hata hivyo,watasimamiwa na polizi kuanzia saa sita kamili hadi na dakika tano.

Aliongeza kuwa kwa upande wa madereva wa magari ni  marufuku kuendesha gari huku akiwa amelewa kwani  kufanya hivyo ni kosa.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.