Na Mwanajuma Abdi, DAR ES
SALAAM
WAZIRI wa Uchukuzi Tanzania,
Dk. Harrison Mwakyembe, amewafukuza kazi wafanyakazi sita wa Shirika la Reli (TRL)
kwa wizi wa mafuta na fedha za tiketi za treni na kumuagiza Kamanda wa Polisi
kuwakamata mara moja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Alitoa kauli hiyo jana, wakati alipokuwa
akihutubia mkutano wa wafanyakazi wa TRL jijini hapa, ambapo alisema shirika
hilo limekuwa likipata hasara kubwa kutokana na wizi wa mafuta uliokithiri na
kuliibia fedga za mauzo ya tiketi halali
wanazotozwa abiria.
Watumishi wengine sita wamepewa
barua za kusimamishwa kazi.
Aliwataja waliofukuzwa kazi na
wanatakiwa wapelekwe rumande kwa ajili ya kupandishwa mahakamani ni pamoja na
Stanley Makunja, Stanley Endrew, Jason Mosesn wa Tabora, B Looga, Edward
Benedeto na Lucy Ntinga, ambae ni mwanamke pekee katika sakata hilo.
Alisema serikali haitavumilia
wizi huo, ambao unafanyika kweupe ambao watu hao wanalisimamisha treni njiani
kwa ajili ya kuiba mafuta, hivyo alitoa wito wa jeshi la polisi kuwafikisha
mahakamani watuhumiwa hao.
Hata hivyo, aliuagiza uongozi
wa TRL kuhakiki mali za wafanyakazi waliokufuzwa kazi na ikithibitika wana mali
nyingi bila ya kuzitolea maelezo zipigwe mnada ili fedha zingizwe katika shirika
hilo.
Alisema mbali ya wizi wa mafuta lakini alidokeza
mtindo wa uuzaji wa tiketi kihalali za treni kwa abiria zipo teketi zimeuzwa
kwa shilingi 61,200 lakini katika risiti ya kopi inasomeka shilingi 16,800
zinazoingia TRL.
“Tiketi imeuzwa kwa shilingi
50,200 kwa mteja halali lakini TRL imeingia shilingi 13,600 na nyengine imeuzwa
kwa shilingi 74,400 lakini katika kopi ya risiti ambayo fedha imeingia ni
shilingi 13,600 na kuna tiketi imeuzwa kwa shilingi 57,600 lakini fedha
iliyoingia shirika ni shilingi 6,700, jambo ambapo mchezo huu umechezwa kwa
kipindi cha miaka mitano mpaka 10, na wanachukua robo tatu wa kile
kinachoingizwa katika mapato ya serikali,” alisema.
Aidha alisema kamati ya
wataalamu wanne iliyoundwa wakiwemo SUMATTA, TRL na Bodi ya wahandisi iongezwe
watu wawili ili waweze kuchunguza mabehewa mapya yanayoanguka, sambamba na
kwenda nchi India yanapotengenezwa kwa ajili ya kuangalia ubora wake, ambapo
yakithibitika kuwa hayafai yazuiliwe huko yasiingie nchini.
Alifahamisha kuwa, mabehewa 125
ya kokoto yameingizwa na yanatarajiwa mengine 174 yataingizwa nchini , hivyo
jopo la kamati hiyo lifike kuyakaguwa ubora wake kabla ya kuingia Tanzania.
Hata hivyo, aliitaka Bodi ya
Wakurugenzi na uongozi wa TRL kusitisha mikataba yote iliyoingia na kampuni
nyengine ili kazi hizo zifanywe na wafanyakazi kwa ajili ya kuokoa fedha za
umma zisitumike vibaya na kusababisha kujiendesha kwa hasara.
Mapema Katibu Mkuu, Erasto John
alisema mabehewa mapya ya treni yaliyoingizwa awamu ya kwanza ni mabovu
yanavunjika kama muhogo lakini pia yaliyofuata nayo ni mabovu hayapo katika
kiwango.
No comments:
Post a Comment