Wapenzi wa mchezo wa Mpira wa migu Zanzibar wakisubiri kwa hamu mpambano wa Kombe la Mapinduzi Kati ya Simba na Mtibwa Sugar, unaotarajiwa kufanyika usiku huu kuazia saa 2:15 usika katika uwanja wa Amaan.
Kwa sasa timu ya Simba ikiwa uwanjani ikipasha viungo kusubiri pambano hilo kwa hamu kulipiza kisasi cha kufungwa na Mtibwa Sugar katika Mchezo wa kirafiki uliofanyika mjini Dar-es-Salaam kwa mabao 4--1.
Nacho kikosi cha Mtibwa Sugar wakiwa uwanjani wakifanya mazoezi ya kujipasha moto kusubiri kukabiliana na Simba katika mchezo wao wa Ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi mchezo unaofanyika usiku huu.
Katika michezo ya Utanguliza wa Kombe la Mapinduzi michezo iliofanyika jioni saa tisa timu ya JKU imeshinda dhidi ya timu ya Mafunzo kwa mabao 2--0.
Mchezo wa jioni kati ya Polisi na Shaba timu ya Polisi imeshinda mchezo huo kwa bao 1--0.
Katika mchezo wa Usiku huu timu ya Simba ikiongoza na Kikosi chake No 1
Golikipa Manyika Peter, Hassan Kessy, Mohammed Hussein, Hassan Issiaka, Abdulllazizi Makame, Awadhi Juma, Elias Maguli, Said Ndemba, Ibrahim Hajib, Singano Ramadhani na Abdi Banda. hicho ni kikosi cha Simba kitakachoaza mpambano na Mtibwa Sugar usiku huu katika Kombe la Mapinduzi.
Wachezaji wa hakiba Denis Richard, William Lucian, Nassor Masoud,Abdallah SEseme, Shaban Kisiga Ibrahim Twaha, Issa Rashid na Dan Sserunkuma.
Timu ya Mtibwa Sugar itaaza mchezo huo na wachezaji wake Golikipa Said Mohammed, Said Mkopi, Divid Luhende, Ali Shomari,, Salim Mbonde, Henry Joseph, Ali Suleiman, Mzaramu Yassin, Ame Ali,Ibrahim Rajab, Jamal Mnyate.
No comments:
Post a Comment