Habari za Punde

Serekari Tayari Imeshayafanyia Matengenezo ya Nyumba za Wazee Pemba na Unguja.

Na Miza Othman- Maelezo
Waziri wa  Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohammed amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kipindi chote cha utekelezaji wa awamu ya saba imejipanga vizuri katika suala zima la kukarabati na kuzifanyia matengenezo makubwa Nyumba za Wazee zilizopo Sebleni  Unguja na Limbani kwa  Pemba.

Ameyaeleza hayo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi, Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibzr wakati alipokuwa akijibu Suala la Mh.Jaku Hashim Ayoub alietaka kujua mpango wa Serikali  wa kuyakarabati majengo hayo ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.

Amesema Wizara yake tayari imeshazifanyia matenganezo makubwa nyumba mbili, Ukumbi  uliop nyumba za  wazee Sebleni na kujenga ukuta uliozunguuka eneo lote la Nyumba hizo.

“Serikali imefanya ukarabati  mkubwa  wa miundombinu ya maji na umeme ili kuhakikisha Wazee wanapata huduma hiyo bila ya matatizo”, aliongeza Waziri Zainab.

Aidha  amesema Serikali imeamuwa kuwapatia  wazee milo mitatu kwa siku na kuwapatia posho la shilingi Arubain Elfu (40,000/=) kwa ajili ya matumizi yao madogo madogo, chakula na posho hizo hutolewa sawa kwa wazee wote waliopo Sebleni na Limbani Pemba.


Hata hivyo ameeleza kuwa kwa upande wa nyumba za wazee za Limbani-Pemba, Wizara tayari imeshachukuwa hatuwa ya kuandaa makisio ya matengenezo yote yanayo hitajika ikiwemo kujenga uzio pamoja na kuzifanyia ukarabati nyumba na kujenga miundo mbinu mipya ya maji na umeme.

“Kinacho subiriwa hivi sasa ni kupata fedha kwa ajili ya mradi huo, nia ya Serikali ni kuzifanyia ukarabati nyumba zote za Sebleni na Limbani ili kuwaweka wazee wetu katika mazingira yaliyo bora zaid na kujenga ustawi wao kwa jumla”, alisisitiza Waziri.

Aidha amesema suala la kuwapati vipando wahudumu wa nyumba hizo   ikiwemo vespa na baskeli viko katika bajeti ya Wizara yake na wakati wowote wakipata fedha suala hilo litatekelezwa kwa kila anaestahiki kupatiwa usafiri wa aina hiyo ili kuleta ufanisi wa kazi zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.