Habari za Punde

Serikali yapokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka kwa Serikali ya China

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB)  akibadilishana hati ya makabidhiano ya vifaa vya michezo na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiana vifaa hivyo leo jijini  Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Balozi wa China hapo nchini Lu Youqing na Mwakilishi Mkuu wa Wafanyabiashara kutoka China waishio nchini  Lin Zhiyong. Jumla ya vifaa kumi na nne vimetolewa ambavyo ni Roboti ya kujifunzia mpira wa Meza, Kifaa cha kupimia upepo kwa ajili ya Riadha,Nyavu ya mpira wa Meza, Mashine ya kupimia Uzito,Ulingo wa Ngumi,Kompyuta,Printa, Radio Call, mashine ya kutafsirina kuhesabu matokeo katika riadha na nyaya za umeme vyenye thamani zaidi ya 200.
Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabibidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa Serikali ya Tanzania vilivyopokelewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB)  akicheza Mpira wa Meza na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiwa msaada wa vifaa vya michezo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing akielezea namna mtambo wa Radio Call unavyofanya kazi, katika mwenye blauzi ya kitenge Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara, na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda
Ulingo wa kisasa uliokabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China leo jini Dar es Salaam.kwa ajili ya michezo ya Ngumi na Kick Boxer
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara MB) akibadilishana hati ya makabidhiano ya vifaa vya michezo na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing (kulia) wakati wa hafla ya kukabibidhiana vifaa hivyo leo jijini  Dar es Salaam.(Picha na Frank Shija)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.