Habari za Punde

Makunduchi kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake

Wadi za Makunduchi zimepania kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake. Katika kikao cha pamoja kati ya wadi za Makunduchi na Manispaa ya Kiruna kilichofanyika nyumbani kwa Mw. Hafith mtaa wa Kwaboko, pande hizo mbili zimekubaliana kuanzisha mradi wa kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake. Kwa mujibu wa mkuu wa mradi wa mashirikiano kati ya pande hizo mbili, ndugu Mohamed Muombwa pande hizo mbili zitatembeleana kujifunza uzoefu. Kwa upande wa wadi za Makunduchi ujumbe wa watu watano unategemewa kuondoka hivi karibuni kwenda Kiruna, Sweden. Ujumbe huo utajumuisha polisi, daktari, mratibu wa masuala ya wanawake, mkuu wa mradi na mwanajamii mmoja. Katika picha upande wa kukia ni ndugu Ove, Kennethm Jenny akifuatiwa na mwalimu Hafith.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.