Habari za Punde

Mwili wa Marehemu Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin Ukumbi wa Baraza Chukwani Zanzibar.

Mwili wa marehemu Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin ukiwa mbele ya ukumbi wa Baraza kwa ajili ya kutowa heshima za mwisho na kuuaga kwa Wananchi na Wajumbe waliofika katika ukumbi huo Chukwani Zanzibar 
Waheshimiwa Wabunge na Wawakilishi na Wananchi wakishiriki katika dua ya kuuaga mwili wa marehemu Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar Salmin Awadh Salmin. aliyefariki hafla jana 19-2-2015 baada ya kuugua hafla akiwa katika kazi zake za kawauidi Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Shekh Noman Thabit Jongo akitowa mawaidha wakati wa kuuaga mwili wa marehemu iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia mawaidha yakitolewa na Shekh Naman Thabit Jongo, akitowa nasaha za dini kwa wananchi waliohudhuria katika kuuaga mwili wa marehemu iliofanyika katika ukumbi wa baraza.
               Waheshimiwa wakiwa na majonzi wakifuatilia mawaidha yaliokuwa yakitolewa
Wajumbe wakiwa na simazi ya kuondokewa na Mwakilishi mwezao wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin, kilichotokea hafla jana mchana.
Naibu Waziri wa Fedha Tanzania Mhe Malima wakiwa katika ukumbi wa Baraza akifuatilia mawaidha yaliokuwa yakitolewa wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin.

Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa na majonzi ya kufiwa na mmoja wa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar Salmin Awadh Salmin, wakisikiliza mawaidha yaliokuwa yakitolewa na Shekh Noman Thabit Jongo,
Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi wakishiriki katika kuuaga mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin iliofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani. 
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis akisoma dua kumuombea marehemu Salmin Awadh Salmin iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad , akijumuika na Wawakilishi na Wabunge katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin iliofanyika katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Waheshimiwa Wabunge na Wawakilishi wakijumuiya katika dua ya pamoja ya kuuombea mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi
Wawakilishi wakijumuika katika dua iliokuwa ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh Khamis Haji Khamis 
Waheshimiwa Wawakilishi wakiwa na majonzi ya kuondokewa na Mwakilishi mwezao hafla jana wakiwa katika maombolezi katika ukumbi wa Baraza ulipoletwa kuuagwa na Wajumbe na Wananchi wengini ukumbini hapo.
Waheshimiwa Wabunge na Wawakilishi wakihudhuria hafla ya kuuaga mwili wa Marehemu Salmin Awadh Salmin ulipofikishwa katika ukumbi wa baraza Chukwani Zanzibar.

Askari wa Baraza la Wawakilishi wakiwa wameubeba mwili wa marehemu Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe Salmin Awadh Salmin,wakitoka katika ukumbi wa baraza baada ya kumaliza kutoa dua 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakitoka ukumbi wa Baraza baada ya kumalizika kwa dua maalum ya kumuaga aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe Salmin Awadh Salmin.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitowa ukumbi wa Baraza baada ya kumalizika kwa Dua ya kuuombea mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, iliofanyika katika ukumbi huo kulia Mwakilishi wa Jangombe Mhe Suleiman Othman Nyanga , Mwakilishi wa Uzini Mhe Mohammed Raza na Mwakilishi wa Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, wakitoka ukumbi wa baraza baada ya kumalizika kwa Dua maalum ya kumuaga marehemu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimaia na Waziri Mkuu Mstaaf wa Tanzania Mhe Edward Lowasa wakiwa katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi walipohudhuria katika hafla ya kuuaga mwili wa marehemu na kusoma dua.
Shekh Noman Thabit Jongo akiongoza sala ya kumsalia marehemu Salmin Awadh Salmin aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar aliyefarika jana hafla akiwa katika kazi zake za Kichama Afisi Kuu Kisiwandui Zanzibar.
Wahesshimiwa Wajumbe wa Bdaraza la Wawakilishi Zanzibar wakiitikia dua baada ya kuusalima mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin katika Masjid Taqkua uliopo katika viwanja vya Baraza Chukwani. dua ilioongozwa na Shekh, Noman Thabit Jongo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.