Habari za Punde

Ngoma ya Msewe kutoka Zanzibar Yatia Fora katika Maonesho ya Sanaa Nchini Oman

 Hussen Ferej akiwajibika jukwaani wakati Watanzania walipokuwa wanatumbwizaNgoma aina ya “Kitua tua” katika Jukwaa kuu la Maonesho ya Kimatifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
 Hussen Ferej akiwajibika jukwaani wakati Watanzania walipokuwa wanatumbwizaNgoma aina ya “Kitua tua” katika Jukwaa kuu la Maonesho ya Kimatifa ya Sanaa Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
 Wasanii wa Ngoma ya Msewe kutoka Tanzania wakitumbuiza katika Jukwaa kuu kwenye Maonesho yanayoendelea ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni,Muscut –Oman.Wasanii hao watakuwa wakitoa burudani hiyo kwa wiki mbili

Baadhi ya Mashabiki wakitazama burudani iliyokuwa ikitolewa na Wasanii kutoka nchi tofauti duniani zinazoshiriki Maonesho Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni, nchini Oman
 Wasanii wa Ngoma ya Msewe kutoka Tanzania wakitumbuiza katika Jukwaa kuu kwenye Maonesho yanayoendelea ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni,Muscut –Oman.Wasanii hao watakuwa wakitoa burudani hiyo kwa wiki mbili
Wasanii kutoka Ufaransa nao wakitoa burudani ya aina yake katika Jukwaa kuu la Maonesho yanayoendelea ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni,Muscut –Oman. 
India ni miongoni mwa Nchi zinazoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na 

Utamaduni,yanayofanyika Muscut –Oman.Wasanii wa kike wa India wakitoa burudani ya 

kiutamaduni wa kihindi katika Jukwaa la Maonesho hayo
Baadhi ya Mashabiki wakitazama burudani iliyokuwa 

ikitolewa na Wasanii kutoka nchi tofauti duniani zinazoshiriki 

Maonesho Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na 

Utamaduni, nchini Oman(Faji Mjaka Oman)

4 comments:

  1. Tumepoteza utaifa na sasa munatupotezea mpaka ngoma na tamaduni zetu. Msewe hautoki Tanzania. Msewe ni ngoma ya asili ya visiwa vya Zanzibar, hususan Pemba. Waandishi wa habari uchwara!!!!

    ReplyDelete
  2. Ndo hapo , wambie hawa jamaa wazushi kweli kweli yaani wameing'ang'ania Zenjbar yetu na utamaduni wetu eti wanajifanya tamaduni kutoka Tanganyika dah hatar kweli aloo.

    ReplyDelete
  3. Msiwalaumu wandishi wao huandikiwa wa wenye Uwezo wa kuwawezesha na kuto wawezesha ,kwa mana hiyo ikiwa watandika vilivyo kuna hatari ya kupoteza kinachowapatia chajiyo ,wakati wa wandishi wakuandika uhalisi bado haujafika kwetu .

    ReplyDelete
  4. Hili suala la utamaduni wa visiwani Unguja na Pemba ni la kusikitisha kuona unapotezwa kwa makusudi.Katika kipindi cha awali ya mapinduzi,zikisikika ngoma za kiasili kwenye vipindi vya redio,sherehe za kitaifa,na zile za kidini kama eid.Tusipo liangalia hili basi na huu msewe utakuwa ni historia.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.