Habari za Punde

Dk Shein Aungana wa Wananchi katika Mazishi ya Mwakilishi wa Magomeni Salmin Awadh Makunduchi Zanzibar.


 
 Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamisi Haji Khamis akiongoza Sala ya kuusalia mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin, katika masjid Muhammad Mombasa kwa Mchina, katika Sala hiyo amehudhuria Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk. Amani Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, na Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa Tanzania.   
Waumini wa Dini ya Kiislam wakiusalia mwili wa Marehemu Salmin Awadh Salmin, katika Masjdi Muhammed Mombasa kwa Mchina. 
Shekh Othman Maalim akisoma dua baada ya kuusalia mwili wa marehemu Salmi Awadh, katika Masjid Muhammed Mombasa kwa Mchina na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Zanzibar na Nje ya Zanzibar.

Waumini wa Dini ya Kiislamu wakiitikia dua baada ya kuusalia mwili wa marehemu katika Masjid Muhammad Mombasa kwa Mchina 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal. akisalimiana na Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume baada ya kusalima maiti katika Masjid Muhammad mombasa.
Wananchi wa Zanzibar wakishiriki katika Mazishi ya aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe. Salmin Awadh Salmin yaliofanyika katika Masjid Muhammad Mombasa kwa Mchina 
Asakari wa Baraza la Wawakilishi wakibeba jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiwa katika Kijiji cha Kijini Makunduchi Wilaya ya Kusinu Unguja tayari kwa mazishi hayo.
Wananchi wakiwa makaburimi katika mazishi ya Mwakilishi wa Magomeni Zanzibar katika Kijiji cha Kijini Makunduchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiongoza mazishi ya mwakilishi wa magomeni yaliofanyika katika Kijiji cha Kijini Makunduchi Unguja Wilaya ya Kusini Unguja,  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akishiriki katika mazishi ya marehemu Salmin Awadh Salmin, aliyekuwa Mwakilishi ya Jimbo la Magomeni na Mnadhimu wa CCM katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, akiweka mchanga kaburini
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Saimin Awadh Salmin wakati wa maziko yake yaliofanyika Kijini Makunduchi. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiweka mchanga katika kaburi baada ya kuzikwa mwili wa Marehemu Salmin Awadh Salmin katika kijiji cha kijini makunduchi. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg. Vuai Ali Vuai, akiweka mchanga kaburini.wakati wa maziko ya mwakilishi wa magomeni Zanzibar.  
         Waziri Mkuu Mstaaf wa Tanzania Mhe Edward Lowasa akishiriki katika mazishi ya mwakilishi wa magombeni yaliofanyika kijiji kwao kijini makunduchi Zanzibar, akiweka mchanga katika kaburi.
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Mark Mwandosa akishiriki katika mzishi hayo akiweka mchanga kaburini wakati wa mazishi hayo yaliofanyika katika Kijiji cha Kijini Makunduchi Zanzibar.


Shekh Hassan Kanji akisoma dua ya kumsomaa maiti wakati wa mazishi yaliofanyika katika makaburi ya Kijini Makunduchi Zanzibar.
Waheshimiwa Viongozi wakiitikia dua baada ya aziko ya mwakilishi wa magombeni yaliofanyika Kijiji kwao Kijini Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja. 
                                            Waheshimiwa wakishiriki katika kuitikia dua
                            Wananchi wakishiriki katikac dua ya kumuombea marehemu.
                           Wananchi wakishiriki katikac dua ya kumuombea marehemu.


















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.